

Mhitimu wa Shahada ya Umahiri ya Mawasiliano ya Umma katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Ndg. Ahmed Sagaff amechukua na kurejesha fomu ya kuomba ridhaa kuteuliwa kuwania ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi katika Jimbo la Dodoma Mjini kwenye uchaguzi mkuu 2025.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini hapa, Sagaff ameahidi kusimamia utekelezaji wa ahadi zilizopo kwenye Ilani ya uchaguzi ya CCM 2025-2030 katika jimbo hilo ili kuunga mkono jitihada za serikali za kustawisha maisha ya wakazi wa Dodoma Mjini na Watanzania wote kwa ujumla.
“Nakwenda kuomba ridhaa ya kuendeleza mema yaliyofanywa na Ndg. Anthony Mavunde, nitaomba idhini ya kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan katika kutimiza maono yake, na nitaomba ruhusa ya kuwawakilisha kikamilifu wakazi wa Dodoma Mjini,” ameahidi.
Kabla ya kuingia rasmi kwenye siasa, Sagaff amehudumu kwenye Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa muda wa miaka mitano (2020-2025) kama Afisa Habari akiwa na majukumu ya kufuatilia na kutangaza utekelezaji wa miradi, programu, sera, na mipango ya serikali.
“Katika utumishi wa umma nimejifunza namna serikali inavyopunguza umasikini, inavyoimarisha usawa wa kijinsia, na mengine mengi, kikubwa zaidi nimejifunza kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi,” amedokeza.
Kitaaluma, Sagaff ni mwanahabari aliyepata elimu yake katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Chuo Kikuu Tumaini (TUDARCo), na Chuo cha Uandishi wa Habari Zanzibar (ZJMMC).
“Mwenyezi Mungu anasema kwamba elimu tuliyopewa wanadamu ni ndogo sana, hivyo hatupaswi kujikweza bali tunapaswa kuzitumia elimu zetu katika kuwatumikia wanadamu wote na kuhakikisha kwamba dunia inaendelea kuwa sehemu salama ya kuishi,” ameeleza.
RAIS MWINYI ATEMBELEA BANDA LA NISHATI MAONESHO YA SABASABA
REA YAJIZATITI KUFIKISHA LENGO LA TAIFA KWENYE NISHATI SAFI YA KUPIKIA
CPA KASORE ASISITIZA UMUHIMU WA KUFUNDISHA MAFUNZO YA UFUNDI STADI KWA WATOTO ILI WAWEZE KUJITEGEMEA
TPDC YAJIVUNIA MAFANIKIO YAPATA TUZO SABASABA.
TANESCO YATOA MAJIKO YA UMEME KWA WANANCHI SABASABA.
Maiko Salali achukua fomu ya ubunge Jimbo la Mpwapwa
SERIKALI IMEPUNGUZA TOZO KATIKA ZAO LA KAHAWA KUTOKA 17 HADI 5.
Mkoa wa Katavi umeendelea kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM)
UDOM KUJA NA TEKNOLOJIA MPYA YA KUUZA VIMIMINIKA.
AMANZI NA BABU TALE USO KWA USO JIMBONI