Mkoa wa Katavi umeendelea kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

Mkoa wa Katavi umeendelea kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM)

Mkoa wa Katavi umeendelea kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) ambapo Mwaka 2021 Mkoa ulikuwa na jumla ya vituo 102 vya kutolea huduma za Afya na hadi kufikia Mwezi Juni, 2025 Mkoa una Jumla ya vituo vya kutolea huduma za Afya 161 ikiwa ni ongezeko la vituo 59, Sawa na ongezeko la asilimia 36.64

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
03 Jul 2025
Mkoa wa Katavi umeendelea kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM)

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya Serikali ya awamu ya Sita tarehe 03 Julai 2025 Katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo jijini Dodoma.

Aidha amesema kuwa Zahanati zimeongezeka kutoka 80 mwaka 2021 hadi 127 mwaka 2025 sawa na ongezeko la zahanati 47, Vituo vya Afya vimeongezeka kutoka 17 mwaka 2021 hadi kufikia 28 mwaka 2025 sawa na ongezeko la vituo 11 sawa na ongezeko la asilimia 39 pamoja na Ukamilishaji wa Hospitali 4 za Wilaya na ukarabati wa hospitali Kongwe ya Manispa ya Mpanda umekamilika.

Aidha Kwa upande wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa fedha Bilioni 18.386 zilizopokelewa kwa kipindi cha miaka MITANO zimesaidia kukamilisha;Miundombinu ya jengo la ‘Wing A” lenye huduma za wagonjwa wa nje, huduma za mama na mtoto, Vipimo vya radiologia na vyumba vya upasuaji.

"Ujenzi wa jengo la ‘Dialysis” (Huduma ya kusafisha Damu) umekamilika kwa asilimia 100 na huduma zimeanza kutolewa, Ujenzi wa jengo la huduma za dharura (EMD), Ujenzi wa jengo la wagonjwa mahututi (ICU), Ujenzi wa nyumba ya mtumishi,Ununuzi wa mashine ya CT-Scan, Ununuzi wa mashine mbili za kisasa za mionzi (digital X-Ray) pamoja na Ununuzi wa Vifaa tiba mbalimbali"

"Mafanikio makubwa ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ni wananchi kupata huduma kirahisi, kupunguza kusafirisha wagonjwa kwenda nje kwa kuendelea kupata huduma za ki-bingwa ambazo ni Huduma za kibigwa za upasuaji, Huduma za kibingwa za mifupa, Huduma za kibingwa za afya ya uzazi, Huduma za kibingwa za sikio, pua na kinywa, huduma za kibingwa za Magonjwa ya Ndani pamoja na huduma za kibingwa za magonjwa ya dharura"

Aidha Mwaka 2021 Mkoa ulipokea kiasi cha Tshs 2,980,556,000.00 za ununuzi wa dawa, Vifaa, Vifaa tiba na vitendanishi na kwa mwaka 2024 mkoa umepokea kiasi cha Tshs 3,380,560,000.00 Kumekuwa na ongezeko la bajeti ya dawa kwa kiasi Tshs 400,000,000.00 sawa na asilimia 11.8. Hadi kufikia mwezi Juni 2025 wastani wa upatikanaji wa dawa ni asilimia 94

Sanjari na hayo kumekuwa na ongezeko la vituo vilivyoboreshwa vyenye uwezo wa kutoa huduma za dharura ikiwa ni pamoja na huduma za upasuaji kwa kina mama wajawazito kutoka vituo 8 Mwaka 2021 hadi kufikia vituo 14 Mwaka 2025, Aidha, Wajawazito wanaojifungulia kwenye vituo vya huduma wameongezeka mwaka hadi mwaka. Kina mama 40,269 mwaka 2021 hadi kufikia kina mama 48,322 mwaka 2025.

Aidha  Kumekuwa na ongezeko la magari ya wagonjwa (Ambulance) kutoka 10 mwaka 2021 hadi 17 mwaka 2025, Magari haya yamerahisisha usafirishaji wa Wagonjwa wanaohitaji huduma za rufaa kutoka ngazi ya Zahanati na Vituo vya Afya Kwenda Hospitali za Wilaya pamoja na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa

Kwa upande wa Sekta ya maji Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mpanda (MUWASA) inatoa huduma ya Maji katika Kata 15 za Manispaa ya Mpanda ambapo katika kipindi cha uongozi wa Rais wa awamu ya Sita, Mkoa umeendelea kutekeleza miradi MITANO yenye thamani ya Shilingi bilioni 32,163,080,399.89 ambayo ikikamilika itaongeza upatikanaji wa Maji kwa zaidi ya asilimia 100.

"Mkoa unaendelea kutekeleza mradi wa usamabazaji Maji kutoka Bwawa la Milala unaotekelezwa chini ya mpango wa ujenzi wa mradi wa Maji wa Miji 28,Mradi huu unatarajiwa kuzalisha Maji lita 12,000,000 kwa siku na kunufaisha wakazi wote wa Manispaa ya Mpanda, Hadi kufikia Juni, 2025 hatua ya utekelezaji imefikia asilimia 42 mradi unatekelezwa kwa muda wa miezi 30 kuanzia 11 Aprili, 2023 na unatarajiwa kukamilika Mwezi Oktoba 2025"

Kwa upande wa Maji Vijijini katika kipindi cha uongozi wa Rais wa awamu ya Sita, Mkoa kupitia Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) umepokea jumla ya Shilingi 33,529,634,479.08 (Bilioni 33.352) kwa ajili ya miradi 51 ya Maji vijijini.

"Utekelezaji wa miradi hii imesaidia kuongeza idadi ya watumiaji wa Maji vijijini kutoka asilimia 62.2 mwaka 2021 hadi kufikia asilimia 77.3 Juni, 2025 sawa na ongezeko la asilimia 15.1"

Aidha Mkoa wa Katavi pamoja na Wilaya zake ulikuwa unapata Umeme unaofuliwa katika vituo viwili (2) vilivyopo Mpanda Mjini (MW 7.5) na Mlele (MW 1.44) ambavyo vinatumia mafuta mazito ya dizeli. Halmashauri ya Mpimbwe ilikuwa inapokea Umeme kutokea Sumbawanga ambao ni wa Gridi ya Taifa ya Zambia eneo la Mbala.

Hadi kufikia mwezi Juni, 2025 Mkoa wa katavi umeunganishwa na umeme wa Gridi ya Taifa na umewashwa katika Wilaya ya Mlele, Halmashauri ya Nsimbo na Wilaya ya Tanganyika.

"Gharama za Mradi huu ni shilingi billion 116 kutokea Mkoa wa Tabora 132KV. Mradi umehusisha ujenzi wa njia kubwa ya Umeme ya msongo wa Kilovoti 132 kutoka Tabora hadi Katavi umbali wa kilomita 383 na kujenga vituo viwiwli vya kupoozea Umeme katika eneo la Inyonga kituo chenye ukubwa wa 12MW na eneo la Mpanda kituo chenye ukubwa wa 28MW"

Waziri Ridhiwani Atoa Wito kwa Vijana Kuchangamkia Fursa Zilizopo.

Waziri Ridhiwani Atoa Wito kwa Vijana Kuchangamkia Fursa Zilizopo.

TPDC ,DC CPP na CPTDC ZASAINI MAKUBALIANO UJENZI WA BOMBA LA GESI ASILIA KUTOKA NTORYA HADI MADIMBA.

TPDC ,DC CPP na CPTDC ZASAINI MAKUBALIANO UJENZI WA BOMBA LA GESI ASILIA KUTOKA NTORYA HADI MADIMBA.

TAKUKURU YAWATAKA VIONGOZI WA DINI KUKEMEA RUSHWA.

TAKUKURU YAWATAKA VIONGOZI WA DINI KUKEMEA RUSHWA.

OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA KUTOA ELIMU YA SHERIA ZA UCHAGUZI SABASABA.

OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA KUTOA ELIMU YA SHERIA ZA UCHAGUZI SABASABA.

Watu 36 Wafariki Dunia, Majeruhi 23 Wakimbizwa Hospitali

Watu 36 Wafariki Dunia, Majeruhi 23 Wakimbizwa Hospitali