AMANZI NA BABU TALE USO KWA USO JIMBONI | The Dodoma Post
The Dodoma Post Siasa

AMANZI NA BABU TALE USO KWA USO JIMBONI

Aliyekuwa Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Tawi la Chuo Cha Kodi na Mjumbe wa Seneti ya Mkoa wa Dar es Salaam Mwaka 2021/2022, Amechukua na kurudisha fomu ya Kugombea Ubunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki Leo Tarehe 30/06/2025,

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
01 Jul 2025
AMANZI NA BABU TALE USO KWA USO JIMBONI

Aliyekuwa Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Tawi la Chuo Cha Kodi na Mjumbe wa Seneti ya Mkoa wa Dar es Salaam Mwaka 2021/2022, Amechukua na kurudisha fomu ya Kugombea Ubunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki Leo Tarehe 30/06/2025,

AMANZI ameingia rasmi Kugombea Jimbo Moja na Mbunge aliyemaliza Muda wake katika Jimbo Hilo la Morogoro Kusini Mashariki Mhe. Hamisi Taletale maarufu Babu Tale,

Amanzi ambae ndio kijana pekee aliyechukua fomu katika jimbo hilo akiwa na maono makubwa huku akijidhatiti kuwatumika wananchi pindi atakapopata nafasi hiyo ndani ya chama.

Akizungumza mara baada ya kurejesha fomu amesema vijana ndio nguvu kazi ya taifa hivyo ameona ni muda muhimu kuweza kulitumikia taifa lake

Amesema kutokana na utekelezaji wa ilani ya chama chini ya usimamizi wa Rais Dk Samia Suluhu Hassan katika majimbo mpaka nchi umepelekea kujitathimini na kuona anafaa kuweza kumsadia Rais kuisimamia na kutekeleza ilani ya chama kwa kuwatumikia wananchi.

"Kutokana na demokrasia iliyopo kwenye chama chetu imepelekea mimi kama kijana ambae nimejitathimini na kujipima lakini pia ninauzoefu wa uongozi ndani ya chama kuamua kuchukua fomu ili chama kikinipa ridhaa niweze kuwatumikia wananchi",Amesema Amanzi.

Mpaka sasa Amanzi ni kijana Pekee aliyethubutu Kugombea Ubunge katika Jimbo Hilo la Morogoro Kusini Mashariki.

CHIPUKIZI ACHUKUA FOMU YA UDIWANI KATA YA MWEMBESONGO.

CHIPUKIZI ACHUKUA FOMU YA UDIWANI KATA YA MWEMBESONGO.

Maiko Salali Arejesha Fomu ya Kugombea Ubunge Jimbo la Mpwapwa, Apongeza CCM kwa Ujumuishwaji wa Makundi Maalum

Maiko Salali Arejesha Fomu ya Kugombea Ubunge Jimbo la Mpwapwa, Apongeza CCM kwa Ujumuishwaji wa Makundi Maalum

DWIGHT DANDA KIJANA MDOGO NA MHITIMU WA CHUO KIKUU ATIA NIA UBUNGE KIBAMBA

DWIGHT DANDA KIJANA MDOGO NA MHITIMU WA CHUO KIKUU ATIA NIA UBUNGE KIBAMBA

Katimba aomba ridhaa Ubunge viti maalumu Kigoma

Katimba aomba ridhaa Ubunge viti maalumu Kigoma

SAGAFF AJITOSA KUMRITHI MAVUNDE DODOMA MJINI

SAGAFF AJITOSA KUMRITHI MAVUNDE DODOMA MJINI