RAIS MWINYI ATEMBELEA BANDA LA NISHATI MAONESHO YA SABASABA | The Dodoma Post
The Dodoma Post Nishati

RAIS MWINYI ATEMBELEA BANDA LA NISHATI MAONESHO YA SABASABA

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi leo 7 Julai, 2025 ametembelea banda la Wizara ya Nishati kwenye maonesho ya biashara ya kimataifa maarufu kama sabasaba jijini Dar es salaam

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
08 Jul 2025
RAIS MWINYI ATEMBELEA BANDA LA NISHATI MAONESHO YA SABASABA

RAIS MWINYI ATEMBELEA BANDA LA NISHATI MAONESHO YA SABASABA

*Apatiwa elimu juu ya utekelezaji wa mkakati wa Taifa wa  Nishati safi ya kupikia

* Wizara ya Nishati kuendelea kuweka mazingira mazuri kwa tasisi zake kutekeleza majukumu yake kikamilifu

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi leo 7 Julai, 2025 ametembelea banda la Wizara ya Nishati  kwenye maonesho ya biashara ya kimataifa maarufu kama sabasaba jijini Dar es salaam

Akiwa kwenye banda la Wizara ya Nishati Mhe Mwinyi alipokelewa na Mkuu wa kitengo cha  Mawasiliano Serikalini Bi Neema Chalila Mbuja, ambapo alimweleza juu ya hatua za utekelezaji zilizofikiwa kwenye utekelezaji wa mkakati wa Taifa wa nishati safi ya kupikia na kuongeza kuwa ajenda hiyo ni utekelezaji wa azimio la Mhe Rais Samia kama kinara wa nishati safi ya kupikia.

Amesema Wizara ya Nishati kupitia taasisi zilizopo chini ya Wizara zimekuwa zikitekeleza kwa vitendo ajenda hiyo kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambae ni kinara wa nishati safi ya kupikia kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2034 asilimia 80 ya watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia.

Wizara ya nishati tayari imezindua mikakati miwili ya nishati safi ya kupikia na ule wa mawasiliano ili kuwezesha utekelezaji wa ajenda ya nishati safi ya kupikia kwa vitendo

Wenye malori watakiwa kuweka vifaa vya usalama

Wenye malori watakiwa kuweka vifaa vya usalama

REA Yashukuru Maono ya Rais Samia, Yajipanga Kusambaza Umeme na Nishati Safi Hadi Vitongojini

REA Yashukuru Maono ya Rais Samia, Yajipanga Kusambaza Umeme na Nishati Safi Hadi Vitongojini

EWURA YABORESHA UPATIKANAJI WA HUDUMA KWENYE MITANDAO YAO YA KIJAMII

EWURA YABORESHA UPATIKANAJI WA HUDUMA KWENYE MITANDAO YAO YA KIJAMII

NISHATI YA GESI ASILIA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA NCHI.

NISHATI YA GESI ASILIA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA NCHI.

DKT. BITEKO AZINDUA MKAKATI WA TAIFA WA MAWASILIANO WA NISHATI SAFI YA KUPIKIA.

DKT. BITEKO AZINDUA MKAKATI WA TAIFA WA MAWASILIANO WA NISHATI SAFI YA KUPIKIA.