

Chuo kikuu Dodoma UDOM kimekuja na teknolojia mpya ya uuzaji wa vimiminika kidigital ambapo imekuja kutatua changamoto mbalimbali za wajasiliamali lakini pia kuokoa muda.
Chuo kikuu Dodoma (UDOM) kimekuja na teknolojia mpya ya uuzaji wa vimiminika kidigital ambapo imekuja kutatua changamoto mbalimbali za wajasiliamali lakini pia kuokoa muda.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya 49 ya biashara Sabasaba jijini Dar es salaam julai 3,2025 muhazili Mwandamizi kwenye ndaki ya sayansi za komputa na elimu angavu kutoa UDOM Hassan kilavo amesema kufuatia kasi ya ukuaji wa teknolojia ndio umepelekea chuo hiko kubuni mashine hiyo ya kuuzia vimiminika.
"Hii ni teknolojia ni mpya hapa kwetu tumeianzisha mahususi kwa ajili ya wafanyabiashara wa vimiminika kwani kwa kutumia mashine hii utaweza kuokoa muda na haiitaji muhudumu kwani inaweza kusetiwa na mtu akajihudumia mwenyewe",amesema
Aidha amesema mashine hiyo inatoa huduma ya kidigital kwani inamifumo ya malipo ya kidigital ambapo haiitaji mtu kuwepo ili kupata huduma badala yake mteja anaweza kujihudumia mwenyewe
Sambamba ameongeza kuwa ikiwa mjasiliamali anamtaji wake lakini hana mashine wanaweza kuingia makubalino na kumpatia mashine kwa mkopo au kwa maelewano maalumu.
Amesema kama mtu hana milioni 14 ya kununulia wanaweza kukaa chini na kuongea waone namna ambavyo wanaweza kuweka mikakati ya kulipia mashine hiyo.
“Niwaambie wajasiliamali Sasa hivi tunaenda kiteknolojia zaidi kwa hiyo watu watumie keknolojia kwa ajili ya kurahisisha mambo wanayoyafanya”,Amesema.
Mashine hiyo yakuuzia vimiminika imetengenezwa na chuo kikuu Cha UDOM ambapo zinatengenezwa kutokana na uhitaji wa mtu na aina ya vimiminika vinavyotarajiwa kuuzwa.
BODI YA MKONGE TANZANIA YATANGAZA FURSA KWA WATANZANIA.
SHERIA ZILIZOTAFSIRIWA KWA LUGHA YA KISWAHILI KUTOKA MWEZI AGOSTI.
DCEA:SERIKALI IMEPUNGUZA KASI YA WALAIBU WA DAWA ZA KULEVYA.
ULINZI NA USALAMA BAHARINI UMEIMARIKA;TASAC
VITONGOJI VYOTE 64,359 VITAKUWA NA UMEME IFIKAPO 2030
Maiko Salali achukua fomu ya ubunge Jimbo la Mpwapwa
SERIKALI IMEPUNGUZA TOZO KATIKA ZAO LA KAHAWA KUTOKA 17 HADI 5.
Mkoa wa Katavi umeendelea kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM)
AMANZI NA BABU TALE USO KWA USO JIMBONI
Ubalozi wa Marekani waahidi kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari nchini.