

Serikali imepunguza tozo katika zao la kahawa kutoka idadi ya tozo 17 hadi 5 pamoja na kuhakikisha kahawa inauzwa katika minada rasmi.
Hali hii imesababisha Uzalishaji umeongezeka kutoka tani 53,417 hadi tani 54,203 za maganda kwa mwaka,Bei kwa kilo moja kupanda kutoka Tshs. 1,200 hadi Tshs. 4,200.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajjat Fatma Mwasa wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya Serikali ya awamu ya Sita tarehe 01 Julai 2025 Katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo jijini Dodoma.
Aidha Vikundi vya wanawake, vijana na wenye ulemavu vilivyopewa mikopo ya asilimia 10 isiyo na riba vimeongezeka kutoka 630 hadi 1,370.kiwango cha mikopo iliyotolewa nacho kimeongezeka kutoka Tshs. Bil. 3.23 hadi Tshs. Bil. 9.41.Kupitia mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF), kaya zilizonufaika zimeongezeka kutoka 36,045 hadi 380,035.
Aidha, ruzuku iliyotolewa kwa kaya hizo imeongezeka pia kutoka Tshs. Bil. 16.82 hadi Tshs. Bil. 34.86.Katika mpango wa Mkoa wa kuanzisha mashamba makubwa (block farms) ya kahawa na migomba, vijana 300 wamewezeshwa kuanzisha shamba la kahawa la ekari 300 katika kijiji cha Makongora, Muleba likiwa ni shamba namba moja.Kongani 4 za vijana zimeanzishwa katika Wilaya za Missenyi, Bukoba, Muleba na Kyerwa zilizowezesha vijana 180 kujiajiri na kuajiri wengine.
"Idadi ya biashara rasmi zimeongezeka kutoka 16,376 hadi 25,378 sawa na ongezeko la 55%.Wafanyabiashara wadogo (Machinga) waliotambuliwa katika mfumo rasmi wameongezeka kutoka 1,550 hadi 2,821 sawa na 82% na wamewezeshwa kupata ofisi yao iliyogharimu Tshs. Mil. 35 ambapo Mhe. Rais alichangia Tshs. Mil. 10"
"Wawekezaji katika Mkoa wameongezeka kutoka 175 hadi 275, ambapo Kituo cha Uwekezaji (TIC) kimesajili miradi yenye thamani ya Tshs. Bil. 267.16 inayotoa ajira 11,072."
Aidha Makusanyo yameongezeka kutoka jumla ya Tshs. Bil. 23.6 mwaka 2020/21 hadi Tshs. Bil. 47.2 mwaka 2024/25 kufikia mwezi Mei, 2025 sawa na ongezeko la 100%. ambapo kwa kipindi cha miaka mitano (5) zimekusanywa jumla ya Tshs Bil. 175.8
Aidha ameongeza kuwa Tangu mwaka wa fedha 2024/25 Mkoa umekuwa ukitekeleza miradi ya kimkakati ipatayo 28 kwa kutumia fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri zake.
"Miradi hii itagharimu jumla ya Tshs. Bil. 25.93 na hadi sasa zimeshatengwa katika bajeti (mwaka 2024/25 na 2025/26) jumla ya Tshs. Bil. 11.52 na utekelezaji unaendelea katika hatua mbalimbali"
"Baadhi ya miradi hiyo ni Ujenzi soko la kisasa, Muleba Mjini kwa gharama ya Tshs. Bil. 3 - umefikia 41%, Ujenzi wa shule za michepuo ya kiingereza Katika Wilaya ya Kyerwa Tshs. Bil. 1 iliyofikia 40% na Ngara Tshs. Mil. 530 imefikia 78%, Ujenzi wa ukumbi na maduka ya kisasa Katika Wilaya ya Ngara kwa gharama ya Tshs. Mil. 600 umefikia 35%"
"Ujenzi wa ukumbi na maduka ya kisasa katika Wilaya ya Karagwe kwa gharama ya Tshs. Bil. 2.2. hatua za awali za utekelezaji, Ujenzi wa soko la kisasa la Bunazi/Missenyi kwa gharama ya Tshs. Bil. 16.5. Hatua za kusaini mikataka ya ujenzi na Mkandarasi"
Sanjari na hayo kuna Miradi ya Kimkakati Katika Manispaa ya Bukoba kama Ujenzi wa stendi kuu ya mabasi na Soko kuu la Bukoba - hatua ya kusaini mkataba,Ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilomita 8.8 kwa kiwango cha lami na ujenzi wa kingo za Mto Kanoni zenye urefu wa kilomita 8 - hatua ya kusaini mkataba,Ujenzi wa Stendi ya Mjini Kati kwa gharama ya Tshs. Bil. 1.356 – sawa na utekelezaji wa 80% pamoja na Ujenzi wa masoko ya Kishenge na Machinjioni bajeti imeidhinishwa – utekelezaji utaanza mwaka 2025/26.
BODI YA MKONGE TANZANIA YATANGAZA FURSA KWA WATANZANIA.
SHERIA ZILIZOTAFSIRIWA KWA LUGHA YA KISWAHILI KUTOKA MWEZI AGOSTI.
DCEA:SERIKALI IMEPUNGUZA KASI YA WALAIBU WA DAWA ZA KULEVYA.
ULINZI NA USALAMA BAHARINI UMEIMARIKA;TASAC
VITONGOJI VYOTE 64,359 VITAKUWA NA UMEME IFIKAPO 2030
Maiko Salali achukua fomu ya ubunge Jimbo la Mpwapwa
Mkoa wa Katavi umeendelea kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM)
UDOM KUJA NA TEKNOLOJIA MPYA YA KUUZA VIMIMINIKA.
AMANZI NA BABU TALE USO KWA USO JIMBONI
Ubalozi wa Marekani waahidi kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari nchini.