CPA KASORE ASISITIZA UMUHIMU WA KUFUNDISHA MAFUNZO YA UFUNDI STADI KWA WATOTO ILI WAWEZE KUJITEGEMEA | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

CPA KASORE ASISITIZA UMUHIMU WA KUFUNDISHA MAFUNZO YA UFUNDI STADI KWA WATOTO ILI WAWEZE KUJITEGEMEA

Mkurugenzi mkuu Mamlaka ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi (VETA) CPA Anthony Kasore amesema kuwa mfumo wa elimu nchini umeendelea kuboreshwa ili kutoa fursa kwa kila mtoto kupata elimu ya vitendo itakayomuwezesha kujitegemea na kuleta mabadiliko chanya katika jamii

Sophia Kingimali
By Sophia Kingimali
08 Jul 2025
CPA KASORE ASISITIZA UMUHIMU WA KUFUNDISHA MAFUNZO YA UFUNDI STADI KWA WATOTO ILI WAWEZE KUJITEGEMEA

Mkurugenzi mkuu Mamlaka ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi (VETA) CPA Anthony Kasore amesema kuwa mfumo wa elimu nchini umeendelea kuboreshwa ili kutoa fursa kwa kila mtoto kupata elimu ya vitendo itakayomuwezesha kujitegemea na kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

Akizungumzia na waandishi wa habari julai 7,2025 wakati alipotembelea banda la VETA kwenye maonesho ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba amesema kuna umuhimu wa kuanzisha watoto wadogo kwenye ujuzi wa maisha mapema ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi na kijamii.

"Watoto wadogo wanapaswa kuanza kujifunza ujuzi mapema ili kuwa na ufanisi katika maisha yao ya baadae kwani itapunguza utegemezi",amesema.

Amesema ni lengo lao kubwa kutoa elimu itakayomsaidia kila mtoto wa kitanzania kupata ajira na kujiajiri na kuweza kushiriki katika kukuza uchumi wa nchi.

"Watoto wanapokuwa na ujuzi wa vitendo wanakuwa na uwezo wa kujiajili au kujitegemea na VETA imatoa mafunzo inayowasaidia wanafunzi kuunda na kuuza lakini pia mbinu za ujasiliamali ili waweze kufanya biashara zao kwa ufanisi",Amesema.

Aidha amesema kuwa VETA  imejidhatiti kutoa elimu hiyo ya ujasiliamali ili watoto na vijana waweze kujitengenezea fursa za ajira katika jamii zinazowazunguka.

"Tunajivunia kuona mabadiliko makubwa kwenye mfumo wa elimu nchini sisi VETA  kwa kushirikiana na Serikali tutaendelea kuwakeza katika mafunzo ya ujuzi ili kuhakikisha  vijana wetu wanakuwa na uwezo wa kujiajiri na kuleta mabadiliko chanya katika jamii",Amesema.

TPDC YAJIVUNIA MAFANIKIO YAPATA TUZO SABASABA.

TPDC YAJIVUNIA MAFANIKIO YAPATA TUZO SABASABA.

TANESCO YATOA MAJIKO YA UMEME KWA WANANCHI SABASABA.

TANESCO YATOA MAJIKO YA UMEME KWA WANANCHI SABASABA.

Waziri Ridhiwani Atoa Wito kwa Vijana Kuchangamkia Fursa Zilizopo.

Waziri Ridhiwani Atoa Wito kwa Vijana Kuchangamkia Fursa Zilizopo.

TPDC ,DC CPP na CPTDC ZASAINI MAKUBALIANO UJENZI WA BOMBA LA GESI ASILIA KUTOKA NTORYA HADI MADIMBA.

TPDC ,DC CPP na CPTDC ZASAINI MAKUBALIANO UJENZI WA BOMBA LA GESI ASILIA KUTOKA NTORYA HADI MADIMBA.

TAKUKURU YAWATAKA VIONGOZI WA DINI KUKEMEA RUSHWA.

TAKUKURU YAWATAKA VIONGOZI WA DINI KUKEMEA RUSHWA.