

Mkuu wa Wilaya ya Ludewa ni miongoni mwa viongozi waliopokea maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dk Samia Suluhu Hassan ya kutaka kuenda kusimamia Sekta ya kilimo ipasavyo katika maeneo yao.
Rais Samia ameagiza Kiwanda cha Mbolea cha Intracom cha jijini Dodoma kuimarisha mfumo ya usambazaji wa mbolea hadi vijiji ili kuwawezesha wakulima kupata mbolea kwa gharama ndogo.
Rais Samia ameyasema hayo Juni 28,2025 wakati akizindua Kiwanda cha Mbolea cha Intracom cha jijini Dodoma.
Amesema kikwazo kikubwa ni upatikanaji wa mbolea pamoja na gharama zake, hivyo Serikali wamejipanga kutoa ruzuku za mbolea na wanatoa na sasa wanapata mbolea.
“Sekta hii ni muhimu, Serikali tuko tayari kumfanya mkulima kuzalisha kwa tija ili Serikali iweze kuuza nje kwa bei yenye tija,”amesema.
Amesema kuwa kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Kimataifa itakapofika mwaka 2050 nchi takribani 26 zitakuwa na ongezeko la kwa asilimia 100 ya waliokuwa nao 2015, hivyo upatikanaji wa chakula ni muhimu.
Amesema soko la mbolea bado liko kubwa nchini na kikubwa ni kuwa uzalishaji wa mbolea katika kiwanda hicho unatumia maligjhafi zilizokuwa nchini, hivyo ni mnyororo wa kuongeza thamani kutoka kwa mkulima.
RAIS MWINYI ATEMBELEA BANDA LA NISHATI MAONESHO YA SABASABA
REA YAJIZATITI KUFIKISHA LENGO LA TAIFA KWENYE NISHATI SAFI YA KUPIKIA
CPA KASORE ASISITIZA UMUHIMU WA KUFUNDISHA MAFUNZO YA UFUNDI STADI KWA WATOTO ILI WAWEZE KUJITEGEMEA
TPDC YAJIVUNIA MAFANIKIO YAPATA TUZO SABASABA.
TANESCO YATOA MAJIKO YA UMEME KWA WANANCHI SABASABA.
Maiko Salali achukua fomu ya ubunge Jimbo la Mpwapwa
SERIKALI IMEPUNGUZA TOZO KATIKA ZAO LA KAHAWA KUTOKA 17 HADI 5.
Mkoa wa Katavi umeendelea kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM)
UDOM KUJA NA TEKNOLOJIA MPYA YA KUUZA VIMIMINIKA.
AMANZI NA BABU TALE USO KWA USO JIMBONI