RAIS SAMIA Ameziagiza Wizara ya Fedha,Kilimo Kukaa pamoja na BOT Kuja na Sera ya Taifa. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kilimo

RAIS SAMIA Ameziagiza Wizara ya Fedha,Kilimo Kukaa pamoja na BOT Kuja na Sera ya Taifa.

RAIS Dkt.Samia Suluhu Hassan, ameziagiza Wizara ya Fedha, Wizara ya Kilimo pamoja na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kukaa meza moja ili kuja na Sera ya Taifa ambayo itasimamia utoaji wa mikopo katika sekta ya kilimo nchini.

Moreen Rojas  Dodoma.
By Moreen Rojas Dodoma.
29 Apr 2025
RAIS SAMIA Ameziagiza Wizara ya Fedha,Kilimo Kukaa pamoja na BOT Kuja na Sera ya Taifa.

RAIS Dkt.Samia Suluhu Hassan, ameziagiza Wizara ya Fedha, Wizara ya Kilimo pamoja na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kukaa meza moja ili kuja na Sera ya Taifa ambayo itasimamia utoaji wa mikopo katika sekta ya kilimo nchini.

Rais Samia ametoa maagizo hayo jana tarehe 28 Aprili 2025 jijini Dodoma, alipokuwa  akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa Benki ya Ushirika nchini (COOP).

“Niagize sasa Wizara ya Fedha Benki kuu Wizara ya Kilimo kaeni mzungumze mfikie pahali mje na sera itakayo sijui sera ama niseme muongozo utakaotutoa kwenye hili ombwe la mikopo katika sekta ya kilimo.

“Kuwe kuna sura halisi ambayo Tanzania tunajua sera yetu inayoongozwa na benki kuu katika mikopo ya sekta ya kilimo ni hii na ni nani anafanya nini, TAD anafanya nini benki ya ushirika anafanya nini mabenki mengine yanafanya nini,”amesema

Kwa upande wake Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amemshukuru Rais Dkt.Samia Kwa kukubali kuwekeza kwenye Benki hiyo na kuwa na Imani nayo kwani itaenda Kutatua changamoto za wakulima ambao Kwa kipindi kirefu walikuwa hawana Benki yao.

Naye  Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Stephen Wasira amesema kuzinduliwa kwa Benki ya Ushirika nchini baada ya takribani Miaka 40 kupita ni utekelezaji wa sera ya msingi wa CCM iliyorithiwa kutoka kwa vyama vya ukombozi vya Tanu na Afro- Shirazy Party vilivyokuja kuunda CCM baadae.

Wakati wa salamu za CCM kwenye uzinduzi wa benki hiyo uliofanywa leo na Rais Samia Suluhu Hassan jijini Dodoma, Wasira ameeleza kuwa shabaha ya maendeleo ni kumkomboa mwanadamu kupitia kazi anayoifanya na benki hiyo itawezesha zaidi vyama vya ushirika na mwananchi kupiga hatua za kimaendeleo kupitia sekta ya kilimo.

"Tumekuja hapa kwasababu kazi hii inatimiza azimio la Chama Cha Mapinduzi kuwafanya watanzania wapate  nafuu na kupiga hatua za maendeleo yao siku hadi siku.

"Kazi kubwa ya chama chetu na ajenda yake ambayo haina kikomo ni kuboresha maisha ya watu ili ya leo yawe bora kuliko ya jana na ya kesho yawe bora kuliko ya leo," amesema Wasira.

Kuzinduliwa kwa benki hiyo kulingana naMakamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Stephen Wasira amesema kuzinduliwa kwa Benki ya Ushirika nchini baada ya takribani Miaka 40 kupita ni utekelezaji wa sera ya msingi wa CCM iliyorithiwa kutoka kwa vyama vya ukombozi vya Tanu na Afro- Shirazy Party vilivyokuja kuunda CCM baadae.

Wakati wa salamu za CCM kwenye uzinduzi wa benki hiyo,Wasira ameeleza kuwa shabaha ya maendeleo ni kumkomboa mwanadamu kupitia kazi anayoifanya na benki hiyo itawezesha zaidi vyama vya ushirika na mwananchi kupiga hatua za kimaendeleo kupitia sekta ya kilimo.

"Tumekuja hapa kwasababu kazi hii inatimiza azimio la Chama Cha Mapinduzi kuwafanya watanzania wapate  nafuu na kupiga hatua za maendeleo yao siku hadi siku.

"Kazi kubwa ya chama chetu na ajenda yake ambayo haina kikomo ni kuboresha maisha ya watu ili ya leo yawe bora kuliko ya jana na ya kesho yawe bora kuliko ya leo," amesema Wasira.

Kuzinduliwa kwa benki hiyo kulingana na uongozi wake ni matokeo ya kimkakati na utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025 kulikofanywa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia.

Imeelezwa kuwa lengo la uzinduzi benki hiyo ni kukuza tija katika sekta ya uzalishaji kwenye kufikia malengo na maono mbalimbali kuelekea mpango wa mwaka 2050 unaotaka kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa chakula duniani. uongozi wake ni matokeo ya kimkakati na utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025 kulikofanywa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia.

Imeelezwa kuwa lengo la uzinduzi benki hiyo ni kukuza tija katika sekta ya uzalishaji kwenye kufikia malengo na maono mbalimbali kuelekea mpango wa mwaka 2050 unaotaka kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa chakula duniani.

SERIKALI IMEPUNGUZA TOZO KATIKA ZAO LA KAHAWA KUTOKA 17 HADI 5.

SERIKALI IMEPUNGUZA TOZO KATIKA ZAO LA KAHAWA KUTOKA 17 HADI 5.

Mkuu wa Wilaya Ludewa ashiriki uzinduzi wa kiwanda cha Itracom Dodoma

Mkuu wa Wilaya Ludewa ashiriki uzinduzi wa kiwanda cha Itracom Dodoma

RAIS SAMIA AWAAGIZA WAKUU WA MIKOA KUSIMAMIA KILIMO

RAIS SAMIA AWAAGIZA WAKUU WA MIKOA KUSIMAMIA KILIMO

UZALISHAJI WA MBEGU BORA NDANI YA NCHI UMEONGOZEKA

UZALISHAJI WA MBEGU BORA NDANI YA NCHI UMEONGOZEKA

SEKTA Ya Kilimo Inakabiliwa na Changamoto ya Kupanda kwa Bei ya Mbolea

SEKTA Ya Kilimo Inakabiliwa na Changamoto ya Kupanda kwa Bei ya Mbolea