SEKTA Ya Kilimo Inakabiliwa na Changamoto ya Kupanda kwa Bei ya Mbolea | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kilimo

SEKTA Ya Kilimo Inakabiliwa na Changamoto ya Kupanda kwa Bei ya Mbolea

Sekta ya Kilimo ilikabiliwa na changamoto ya kupanda kwa bei ya mbolea katika soko la ndani kutokana na kupanda kwa bei ya mbolea katika soko la dunia.

Moreen Rojas
By Moreen Rojas
19 Mar 2025
SEKTA Ya Kilimo Inakabiliwa na Changamoto ya Kupanda kwa Bei ya Mbolea

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Bw. Joel Laurent wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa mamlaka hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita  Machi 19, 2025, katika Ofisi za Idara ya Habari - MAELEZO, jijini Dodoma.

Aidha amesema Bei za mbolea nchini zilipanda kutoka wastani wa shilingi 70,000/= kwa mfuko wa kilo 50 hadi kufikia shilingi 140,000/= hadi 150,000/= kwa mfuko ambapo hali hii ilichangia kushuka kwa matumizi ya mbolea, tija na uzalishaji.

"Mpango huu maalumu wa ruzuku ya mbolea uliwezesha kupunguza gharama ya mbolea na kufanya wakulima kununua mbolea kwa bei ya shilingi 40,000/= hadi 80,000/= kwa kutegemea aina ya mbolea na umbali sawa na punguzo la takribani asilimia 50 ya bei"


"kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii, Serikali inatekeleza Mpango wa Ruzuku ya Mbolea kwa kutoa ruzuku kwa wakulima wote na kwa mazao yote nchini"

Aidha amesema kuwa tofauti na ruzuku zilizopita, katika awamu hii ruzuku ya mbolea inatolewa kupitia Mfumo wa Kidijitali wa  Ruzuku ya Pembejeo za Kilimo (Agricultural Inputs Subsidy System) ambao unatumika kusajili wakulima, waingizaji, wazalishaji na mawakala wa mbolea pamoja na kuratibu usambazaji na mauzo.


Aidha Matumizi ya mfumo wa kidijitali katika kusambaza mbolea ya ruzuku umeinufaisha Serikali hususani katika kuwezesha kuanzisha kanzidata ya kuaminika ya wakulima, Mawakala wa mbolea, Waingizaji na Wazalishaji wa mbolea Nchini.


"mfumo huu wa kidijitali umekuwa nyenzo muhimu ya ufuatiliaji na uendeshaji wa biashara ya mbolea nchini kuanzia mbolea inavyoingizwa au kuzalishwa kwenye viwanda vya ndani hadi inapouzwa kwa mkulima katika maeneo mbalimbali nchini.


"Mfumo huu umerahisisha upatikanaji wa takwimu sahihi za matumizi ya mbolea nchini pamoja na kudhibiti udanganyifu  katika  mpango  wa  ruzuku  ya  mbolea"

Sanjari na hayo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita, Mamlaka imeanzisha Maabara ya kisasa ya mbolea ambapo Tanzania inakuwa Nchi ya kwanza katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa na Maabara mahususi ya mbolea,maabara hii inauwezo wa kupima sampuli za mbolea, udongo na tishu za mimea,hii ni hatua muhimu katika kuhakikisha udhibiti wa ubora wa mbolea nchini.

Aidha, maabara hiyo inatarajiwa kutoa huduma kwa nchi jirani zinazotumia bandari za Tanzania, kama vile Malawi, Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Burundi, na Rwanda.

Aidha ameongeza kuwa katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita, biashara ya mbolea nchini imekua kwa kiasi kikubwa ambapo wafanyabiashara wa mbolea waliopewa leseni wameongezeka kutoka 3,069 mwaka 2020/21 hadi 7,302 Februari, 2025.

SERIKALI IMEPUNGUZA TOZO KATIKA ZAO LA KAHAWA KUTOKA 17 HADI 5.

SERIKALI IMEPUNGUZA TOZO KATIKA ZAO LA KAHAWA KUTOKA 17 HADI 5.

Mkuu wa Wilaya Ludewa ashiriki uzinduzi wa kiwanda cha Itracom Dodoma

Mkuu wa Wilaya Ludewa ashiriki uzinduzi wa kiwanda cha Itracom Dodoma

RAIS SAMIA AWAAGIZA WAKUU WA MIKOA KUSIMAMIA KILIMO

RAIS SAMIA AWAAGIZA WAKUU WA MIKOA KUSIMAMIA KILIMO

UZALISHAJI WA MBEGU BORA NDANI YA NCHI UMEONGOZEKA

UZALISHAJI WA MBEGU BORA NDANI YA NCHI UMEONGOZEKA

RAIS SAMIA Ameziagiza Wizara ya Fedha,Kilimo Kukaa pamoja na BOT Kuja na Sera ya Taifa.

RAIS SAMIA Ameziagiza Wizara ya Fedha,Kilimo Kukaa pamoja na BOT Kuja na Sera ya Taifa.