RAIS SAMIA AWAAGIZA WAKUU WA MIKOA KUSIMAMIA KILIMO | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kilimo

RAIS SAMIA AWAAGIZA WAKUU WA MIKOA KUSIMAMIA KILIMO

Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan amewaagiza wakuu wa mikoa nchini kuhakikisha wanakwenda kusimamia Kilimo kwa kuwa ndiyo sekta nyeti na muhimu Kwa taifa.

Moreen Rojas
By Moreen Rojas
28 Jun 2025
RAIS SAMIA AWAAGIZA WAKUU WA MIKOA KUSIMAMIA KILIMO

Rais Samia ameyasema hayo Juni 28 2025 wakati akizindua kiwanda Cha ITRACOM Fertilizers Limited kilichopo Nala jijini Dodoma akiwa sambamba na Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye.

Amesema asilimia 70 ya ajira za watanzania ni katika sekta hiyo na asilimia 25 ya fedha za Kigeni zinatokana na Kilimo huku kikichangia asilimia 30 katika pato la Taifa.

Aidha ametoa rai kwa uongozi wa kiwanda hicho kuhakikisha kuwa wanaimarisha mfumo wa usambazaji wa mbolea kwa wakulima waliopo vijijini

"Nitoe rai kwa uongozi wa Kiwanda cha ITRACOM kuhakikisha kwamba mnaimarisha mfumo wa usambazaji wa mbolea hadi kwa wakulima waliopo vijijini ili waweze kuipata mbolea hii kwa gharama nafuu," amesema Rais Samia.

Amesema mbolea hiyo inapofika Kwa wakulima inatakiwa wawe na maelekezo ya matumizi sahihi kwani Kilimo ndicho kitachangia Kwa kiasi kikubwa katika kuimarisha usalama wa chakula,kupunguza umasikini na kuongeza ajira kwa wanawake na vijana.

Kwa upande wake Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye amesema kupata mbolea ya bei nafuu ni jambo la msingi hivyo uwepo wa kiwanda Cha aina hiyo imepunguza kwa kiasi kikubwa gharama ya mbolea na kuongeza upatikanaji wa chakula.

Waziri wa Viwanda na Biashara Selemani Jafo amesema wizara hiyo itaendelea kuimarisha sekta ya viwanda kwani wakati Rais Samia anaingia madarakani kulikuwa na viwanda 50,000 lakini ndani ya kipindi kifupi wameshajenga viwanda 80,188 na kuwa na ongezeko la viwanda 18,188 na kwamba tayari viwanda 40,000 vimekamilika na vinataka kufunguliwa.

Naye Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema Serikali imetoa Shilingi Bilioni 700 kuwapa wakulima ruzuku ya mbolea na huduma zingine nyingi za Kilimo ambazo wakulima wanapata maendeleo vijijini.

SERIKALI IMEPUNGUZA TOZO KATIKA ZAO LA KAHAWA KUTOKA 17 HADI 5.

SERIKALI IMEPUNGUZA TOZO KATIKA ZAO LA KAHAWA KUTOKA 17 HADI 5.

Mkuu wa Wilaya Ludewa ashiriki uzinduzi wa kiwanda cha Itracom Dodoma

Mkuu wa Wilaya Ludewa ashiriki uzinduzi wa kiwanda cha Itracom Dodoma

UZALISHAJI WA MBEGU BORA NDANI YA NCHI UMEONGOZEKA

UZALISHAJI WA MBEGU BORA NDANI YA NCHI UMEONGOZEKA

RAIS SAMIA Ameziagiza Wizara ya Fedha,Kilimo Kukaa pamoja na BOT Kuja na Sera ya Taifa.

RAIS SAMIA Ameziagiza Wizara ya Fedha,Kilimo Kukaa pamoja na BOT Kuja na Sera ya Taifa.

SEKTA Ya Kilimo Inakabiliwa na Changamoto ya Kupanda kwa Bei ya Mbolea

SEKTA Ya Kilimo Inakabiliwa na Changamoto ya Kupanda kwa Bei ya Mbolea