

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika wakala wa Meli Tanzania (TASAC ) Mohamed Salum ametoa rai kwa wananchi kusoma masomo yanayohusu sekta ya bahari na kupata mafunzo ya kitaalamu kwani bado kuna uhaba wa mabaharia Duniani.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika wakala wa Meli Tanzania (TASAC ) Mohamed Salum ametoa rai kwa wananchi kusoma masomo yanayohusu sekta ya bahari na kupata mafunzo ya kitaalamu kwani bado kuna uhaba wa mabaharia Duniani.
Akizungumza leo, Julai,7 2025 jijini Dar es Salaam kwenye maonesho ya 49 Kimataifa ya Biashara Sabasaba amesema Hadi sasa bado kuna uhaba wa baharia duniani lakini sekta ya bahari ni biashara na inachangia uchumi na ina fursa mbalimbali.
Akizungumzia ushiriki wao kama TASAC Kwenye maonesho hayo amesema wapo hapo kutoa elimu lakini pia kuwajukisha watu fursa zilizopo kwenye sekta ya bahari.
Akizungumzia majukumu ya TASAC amesema jukumu kubwa ni kusimamia mambo yanayohusu usalama wa bahari, meli, maeneo ya bandari na utekelezaji wa Mkataba wa Usalama wa Meli na maeneo ya bandari(ISPS Code).
Poa ameongeza kuwa wanajukumu la kusimamia shughuli za bandari kutoa vibali eneo linalofaa na lisilofaa kwa kujenga bandari.
"Kazi ya TASAC ni pamoja na kukagua vyombo vya usafiri majini, masuala ya kiusalama bandarini na kudhibiti uchafuzi wa mazingira majini unaosababishwa na vyombo vya usafiri majini,"amesema.
RAIS MWINYI ATEMBELEA BANDA LA NISHATI MAONESHO YA SABASABA
REA YAJIZATITI KUFIKISHA LENGO LA TAIFA KWENYE NISHATI SAFI YA KUPIKIA
CPA KASORE ASISITIZA UMUHIMU WA KUFUNDISHA MAFUNZO YA UFUNDI STADI KWA WATOTO ILI WAWEZE KUJITEGEMEA
TPDC YAJIVUNIA MAFANIKIO YAPATA TUZO SABASABA.
TANESCO YATOA MAJIKO YA UMEME KWA WANANCHI SABASABA.
Maiko Salali achukua fomu ya ubunge Jimbo la Mpwapwa
SERIKALI IMEPUNGUZA TOZO KATIKA ZAO LA KAHAWA KUTOKA 17 HADI 5.
Mkoa wa Katavi umeendelea kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM)
UDOM KUJA NA TEKNOLOJIA MPYA YA KUUZA VIMIMINIKA.
AMANZI NA BABU TALE USO KWA USO JIMBONI