

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Ridhiwani Kikwete, ameipongeza Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa mageuzi makubwa iliyofanya katika mashirika ya umma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Ridhiwani Kikwete, ameipongeza Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa mageuzi makubwa iliyofanya katika mashirika ya umma.
Mhe. Kikwete alitoa pongezi hizo Ijumaa, Julai 4, 2025, alipotembelea banda namba 39 (Ukumbi wa Kilimanjaro) katika maonesho ya 49 ya biashara maarufu kama Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
“Tunaishukuru Ofisi ya Msajili wa Hazina chini ya uongozi imara wa Msajili wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, kwa kuwezesha taasisi za umma kuongeza ufanisi wao,” alisema Mhe. Kikwete.
Aliongeza: “Wote ni mashahidi, katika uongozi wa awamu ya sita chini ya Mhe. Rais, Dk. Samia Suluhu Hassan, tumeshuhudia mabadiliko makubwa ya kiutendaji katika taasisi za umma.”
Ofisi ya Msajili wa Hazina imewezesha kuimarika kifedha kwa mashirika ya umma yaliyokuwa na mitaji hasi na yaliyokuwa yanapata hasara mfululizo, ambapo sasa yameweza kuondokana na utegemezi wa ruzuku ya Serikali na kufanikiwa kutoa gawio.
Baadhi ya mashirika hayo ni pamoja na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), ambapo mchango wake katika Mfuko Mkuu wa Serikali ulikuwa Sh10.5 bilioni katika mwaka wa fedha 2024/25.
Pia, katika orodha ya mashirika ambayo kwa sasa yanajiendesha kwa ufanisi ni Shirika la Taifa la Madini (STAMICO), Shirika la Umeme (TANESCO), na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)
Mhe. Kikwete alisema serikali itaendelea kuiunga mkono ofisi ya Msajili wa Hazina katika kuhakikisha safari ya mageuzi inafanikiwa.
“Endeleeni kufanya kazi kwa bidii na pale ambapo kuna mambo mnataka yabadilike katika taasisi ambazo ziko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, hesabuni mmepata ushirikiano kutoka kwetu,” alisema Mhe. Kikwete.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma, Ofisi ya Msajili wa Hazina, Bw. Sabato Kosuri, alisema kumekuwa na ongezeko kubwa la ufanisi kwenye baadhi ya Mashirika kutokana na mageuzi yaliyofanyika na yanayoendelea kufanyika katika Mashirika ya umma.
“Ufanisi umeimarika kwa kiasi kikubwa, mfano mzuri tunauona kwenye Mamlaka ya Bandari,” alisema Bw. Kosuri.
Kwa mwaka huu wa fedha uliopita, pamoja na kuongeza mchango kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali kutoka Sh155.7 bilioni mwaka 2023/24 hadi Sh181 bilioni mwaka 2024/25, matumizi ya kawaida kwa ajili ya shughuli za uendeshaji wa bandari pia yamepungua kwa kiasi cha Sh505.59 bilioni sawa na ufanisi wa asilimia 46.
BODI YA MKONGE TANZANIA YATANGAZA FURSA KWA WATANZANIA.
SHERIA ZILIZOTAFSIRIWA KWA LUGHA YA KISWAHILI KUTOKA MWEZI AGOSTI.
DCEA:SERIKALI IMEPUNGUZA KASI YA WALAIBU WA DAWA ZA KULEVYA.
ULINZI NA USALAMA BAHARINI UMEIMARIKA;TASAC
VITONGOJI VYOTE 64,359 VITAKUWA NA UMEME IFIKAPO 2030
Maiko Salali achukua fomu ya ubunge Jimbo la Mpwapwa
SERIKALI IMEPUNGUZA TOZO KATIKA ZAO LA KAHAWA KUTOKA 17 HADI 5.
Mkoa wa Katavi umeendelea kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM)
UDOM KUJA NA TEKNOLOJIA MPYA YA KUUZA VIMIMINIKA.
AMANZI NA BABU TALE USO KWA USO JIMBONI