UKUAJI WA UCHUMI WA TANZANIA BARA UNAKADILIWA KUFIKIA ASILIMIA 5.8:BoT. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Tanzania

UKUAJI WA UCHUMI WA TANZANIA BARA UNAKADILIWA KUFIKIA ASILIMIA 5.8:BoT.

Kamati ya fedha ya benki kuu ya Tanzania (BoT) imesema Ukuaji wa uchumi kwa Tanzania Bara unakadiriwa kufikia asilimia 5.8 katika robo ya kwanza na asilimia 5.5 katika robo ya pili ya mwaka 2025, ukuaji ambao umechangiwa zaidi na sekta za kilimo, ujenzi na huduma za fedha na bima.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
03 Jul 2025
UKUAJI WA UCHUMI WA TANZANIA BARA UNAKADILIWA KUFIKIA ASILIMIA 5.8:BoT.

Kamati ya fedha ya benki kuu ya Tanzania (BoT) imesema Ukuaji wa uchumi kwa Tanzania Bara unakadiriwa kufikia asilimia 5.8 katika robo ya kwanza na asilimia 5.5 katika robo ya pili ya mwaka 2025, ukuaji ambao umechangiwa zaidi na sekta za kilimo, ujenzi na huduma za fedha na bima.

Hayo yamesemwa  leo Julai 3, 2025 Jijini Dar es Salaam na mwenyekiti wa kamati ya fedha na  Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba wakati akitangaza Riba ya Benki Kuu (CBR) kwa robo ya tatu ya mwaka 2025.

Amesema uchumi wa ndani unatarajiwa kuendelea kuimarika, ambapo ukuaji wake unatarajiwa kufikia asilimia 6.0 na 6.9 katika robo ya tatu na ya nne, mtawalia.

"Kasi hii ya ukuaji inachochewa na uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya reli, barabara, viwanja vya ndege, na viwanja vya michezo kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya CHAN na AFCON, pamoja na uwekezaji unaoendelea katika sekta za kilimo na madini". Amesema

Aidha amesema mfumuko wa bei  kwa Tanzania Bara ulikuwa wastani wa asilimia 3.2 katika robo ya pili ya mwaka 2025, ukiakisi utekelezaji madhubuti wa sera ya fedha na utulivu wa bei za bidhaa zisizo za chakula na zile za nishati.

Hata hivyo, amesema kuwa mfumuko wa bei za chakula uliongezeka kidogo, kutokana na changamoto za usafirishaji zilizosababishwa na mvua kubwa katika baadhi ya maeneo.

Kwa upande wa Zanzibar, amesema mfumuko wa bei ulipungua hadi asilimia 4.2 mwezi Mei 2025, kutoka asilimia 5.3 mwaka mmoja uliopita, hali iliyochangiwa zaidi na kushuka kwa bei za chakula.

Gavana amesema thamani ya shillingi dhidi ya dola ya Marekani ilishuka kwa kasi ndogo ya asilimia 0.2 kwa mwaka ulioishia Juni 2025, ikilinganishwa na kushuka kwa asilimia 12.5 katika katika kipindi kama hicho mwaka jana.

"Utulivu huu umechangiwa hasa na kuongezeka kwa ukwasi wa fedha za kigeni kutokana na mapato ya utalii, na mauzo ya bidhaa nje ya nchi, hususan dhahabu na tumbaku". Ameeleza Gavana Tutuba

Pamoja na hayo Gavana Tutuba amesema utekelezaji madhubuti wa sera ya fedha na usimamizi wa kanuni zinazotaka miamala ya fedha ya ndani ya nchi kufanyika kwa shilingi vimechangia kwa kiasi kikubwa katika kuimarisha utulivu wa shillingi. Vilevile, ongezeko la ununuzi wa dhahabu kutoka ndani ya nchi kwa ajili ya kuongeza akiba ya fedha za kigeni lilichangia kuongeza imani kwa sarafu ya Tanzania.

REA YAJIZATITI KUFIKISHA LENGO LA TAIFA KWENYE NISHATI SAFI YA KUPIKIA

REA YAJIZATITI KUFIKISHA LENGO LA TAIFA KWENYE NISHATI SAFI YA KUPIKIA

MKURUGENZI TASAC AWATAKA WANANCHI KUSOMA MASOMO YANAYOHUSU SEKTA YA BAHARI.

MKURUGENZI TASAC AWATAKA WANANCHI KUSOMA MASOMO YANAYOHUSU SEKTA YA BAHARI.

SHERIA ZILIZOTAFSIRIWA KWA LUGHA YA KISWAHILI KUTOKA MWEZI AGOSTI.

SHERIA ZILIZOTAFSIRIWA KWA LUGHA YA KISWAHILI KUTOKA MWEZI AGOSTI.

WAZIRI KIKWETE AIPONGEZA OFISI YA MSAJILI WA HAZINA.

WAZIRI KIKWETE AIPONGEZA OFISI YA MSAJILI WA HAZINA.

NISHATI SAFI YA KUPIKIA NI AJENDA YA DUNIA, WIZARA INAITEKELEZA KWA VITENDO - DKT. KAZUNGU.

NISHATI SAFI YA KUPIKIA NI AJENDA YA DUNIA, WIZARA INAITEKELEZA KWA VITENDO - DKT. KAZUNGU.