

Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini imetoa rai kwa wananchi kujitokeza kwenye maonesho ya 49 ya biashara sabasaba ili kupata elimu ya sheria zinazosimamiwa na ofisi hiyo hasa katika kipindi hiki tunapoelekea uchaguzi mkuu 2025.
Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini imetoa rai kwa wananchi kujitokeza kwenye maonesho ya 49 ya biashara sabasaba ili kupata elimu ya sheria zinazosimamiwa na ofisi hiyo hasa katika kipindi hiki tunapoelekea uchaguzi mkuu 2025.
Akizungumza na waandishi wa habari leo julai 3,2025 Afisa Sheria Dinna Mcharo amesema ofisi hiyo inasimamia sheria mbalimbali za vyama vya siasa ikiwemo sheria ya vyama vya siasa sura ya 258 lakini pia sheria ya gharama za uchaguzi sura ya 278.
Amesema wameshiriki katika maonesho hayo ili kuendelea kutoa elimu kwa umma ili wapate kujua sheria zinazosimamiwa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi kuu.
"Mimi nitoe rai kwa wananchi wanaokuja kutembelea maonesho haya kuhakikisha wanapita hapa ili waje wapate elimu wajue sheria ziazowasimamia wanasiasa kipindi wanapotekeleza majukumu yao ya kisiasa hasa tunapoelekea uchaguzi mkuu",Amesema.
Aidha ameongeza kuwa ofisi ya msajili wa vyama inamajukumu mengi ikiwemo kusajili na kufuatilia utendaji wa vyama vya siasa kwa mujibu wa sheria lakini piakuratibu shughuli za baraza la vyama vya siasa.
Aidha ameongeza kuwa wanajukumu la kufuatilia mapato na matumizi ya vyama vya siasa lakini kugawa na kufuatilia matumizi ya fedha za ruzuku kwa vyama vya siasa vyenye sifa.
RAIS MWINYI ATEMBELEA BANDA LA NISHATI MAONESHO YA SABASABA
REA YAJIZATITI KUFIKISHA LENGO LA TAIFA KWENYE NISHATI SAFI YA KUPIKIA
CPA KASORE ASISITIZA UMUHIMU WA KUFUNDISHA MAFUNZO YA UFUNDI STADI KWA WATOTO ILI WAWEZE KUJITEGEMEA
TPDC YAJIVUNIA MAFANIKIO YAPATA TUZO SABASABA.
TANESCO YATOA MAJIKO YA UMEME KWA WANANCHI SABASABA.
Maiko Salali achukua fomu ya ubunge Jimbo la Mpwapwa
SERIKALI IMEPUNGUZA TOZO KATIKA ZAO LA KAHAWA KUTOKA 17 HADI 5.
Mkoa wa Katavi umeendelea kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM)
UDOM KUJA NA TEKNOLOJIA MPYA YA KUUZA VIMIMINIKA.
AMANZI NA BABU TALE USO KWA USO JIMBONI