DCEA:SERIKALI IMEPUNGUZA KASI YA WALAIBU WA DAWA ZA KULEVYA. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Biashara

DCEA:SERIKALI IMEPUNGUZA KASI YA WALAIBU WA DAWA ZA KULEVYA.

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya(DCEA) imesema kufuatia juhudi mbalimbali zilizofanywa na serikali imepelekea kupunguza kwa kiasi kikubwa walaibu wa dawa hizo huku akitoa rai kwa wale ambao wameathirika na dawa hizo waweze kujitokeza ili wapate msaada kwani serikali inawatibu bure.

Sophia Kingimali.
By Sophia Kingimali.
05 Jul 2025
DCEA:SERIKALI IMEPUNGUZA KASI YA WALAIBU WA DAWA ZA KULEVYA.

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya(DCEA) imesema kufuatia juhudi mbalimbali zilizofanywa na serikali imepelekea kupunguza kwa kiasi kikubwa walaibu wa dawa hizo huku akitoa rai kwa wale ambao wameathirika na dawa hizo waweze kujitokeza ili wapate msaada kwani serikali inawatibu bure.

Akizungumza leo Julai 5,2025 katika Maonesho ya Biashara ya 49 ya Kimataifa yanayoendelea Sabasaba jijini Dar es Salaam mara baada ya kutembelea Kamishina Jenerali wa Mamlaka hiyo Aretas Lyimo amesisitiza watakaoendelea kukaidi maelekezo ya Serikali watahakikisha hatua za kisheria zinachukua mkondo wake na wataendelea  kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

"Nipende kuwaambia wale ambao bado wanaendelea kufanya biashara ya dawa za kulevya kwamba mkono wa chuma utawafikia ,pumzi ya moto itawafikia na sheria itachukua mkondo wake kwa kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria".Amesema.

Aidha ameongeza kuwa wale wote watakaoendelea kutangaza, kusifia au kuhamasisha matumizi ya dawa za kulevya iwe kwa mavazi, nyimbo au liwe ni kwa jambo lolote lile linaloonesha wanasifia au wanahamasisha matumizi ya adawa za kulevya hatua ya kisheria itaendelea kuchukuliwa.

Amesema na ndani ya sheria kuna vifungu vya sheria hususani kifungu namba 24 kinachoeleza kwamba yeyote yule anayehamasisha matumizi dawa za kulevya anachukuliwa hatua kama wahalifu wengine.

Hivyo amewaomba  Watanzania waachane na biashara ya matumizi ya dawa za kulevya, waachane na uzalishaaji na usambazaji wa dawa hizo lakini wazazi wahakikishe wanalinda watoto wao wasijiingize kwenye matumizi au biashara ya dawa za kulevya ili kuhakikisha tunajenga kizazi imara na uchumi endelevu kwa nchi yetu .

Kuhusu hali ya dawa za kulevya nchini, Kamishna Jenerali Lyimo amesema kwa sasa hali inaendelea kuwa nzuri na inaendelea kuimarika kutokana na operesheni mbalimbali zinazoendelea kufanywa na mamlaka hiyo kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama.

Akizungumza kuhusu Hali ya sasa hivi dawa za kulevya ikiwemo heron na Cocaine zimeadimika kwa kiasi kikubwa hata ukienda kwenye vijiwe ,stendi za basi na maeneo mengine huwezi kukuta wale mateja ambao allizoeleka kuonekana barabarani.

“Sasa hali imekuwa tofauti na hiyo imetokana na Serikali kuamua kuwachukua waraibu ambao wamepelekwa kwenye mfumo wa tiba ,wanapata matibabu na wanaendelea kuimarika na wanarudi katika hali zao za kawaida na wote wanatibiwa bure.”

Awali akieleza ushiriki wa Mamlaka hiyo katika maonesho hayo amesema  lengo ni kuwapa wananchi elimu ili wajue aina ya dawa za kulevya lakini wajue unapokamatwa na dawa za kulevya sheria inasemaje kuhusu dawa hizo.

Amesema kwa  sasa hivi wako katika operesheni maalum ya kuhakikisha wanatoa elimu maalum kwa wanafunzi wa elimu ya msingi sekondari na vyuo lakini pia kufanya operesheni maalum ya kukamata wale wote ambao bado wanaendelea kujihusisha na biashara ya usambazaji na uzalishaji wa dawa za kulevya.

“Lengo ni kuhakikisha kwamba ndani ya kipindi kifupi tunamaliza kabisa tatizo la dawa za kulevya nchini lakini wananchi kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu dawa za kulevya. Wanaoendelea kufanya biashara hizo waweze kuacha na wanaoingia kwenye matumizi ya dawa za kulevya wasiingie kwenye matumizi ya dawa hizo.

“Lakini wale ambao tayari wameingia kwenye matumizi ya dawa za kulevya waweze kupatiwa matibabu na Serikali inatoa huduma za matibabu bure kwa wale ambao wameathiriwa na dawa za kulevya.Lengo la Serikali awamu ya sita ni kuhakikisha walioathiriwa dawa za kulevya wanarudi kwenye afya njema ili tuungane kwa pamoja ili kujenga uchumi wa nchi yetu ya Tanzania.”amesema.

BODI YA MKONGE TANZANIA YATANGAZA FURSA  KWA WATANZANIA.

BODI YA MKONGE TANZANIA YATANGAZA FURSA KWA WATANZANIA.

VITONGOJI VYOTE 64,359 VITAKUWA NA UMEME IFIKAPO 2030

VITONGOJI VYOTE 64,359 VITAKUWA NA UMEME IFIKAPO 2030

FCC YATOA ELIMU YA UTAMBUZI BIDHAA FEKI SABASABA.

FCC YATOA ELIMU YA UTAMBUZI BIDHAA FEKI SABASABA.

Prof.MTAMBO APONGEZA MAANDALIZI YA SABASABA 2025.

Prof.MTAMBO APONGEZA MAANDALIZI YA SABASABA 2025.