

Wakati juhudi za uokoaji na uondoshaji wa miili zikiendelea usiku huu wilayani Same mkoani Kilimanjaro, watu 36 wamethibitishwa kufariki dunia katika ajali mbaya iliyohusisha basi la abiria la kampuni ya Chanel One na basi dogo aina ya Coaster, yaliyogongana uso kwa uso na kuwaka moto.
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Kilimanjaro, Jeremiah Mkomagi, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema taarifa zilizopo kwa sasa ni za awali huku juhudi za uokoaji zikiendelea kufanywa na vikosi vya uokoaji.
"Miili iliyotolewa eneo la tukio mpaka sasa ni 36 na majeruhi 23 ambao wamekimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu. Zoezi bado linaendelea," amesema Kamanda Mkomagi.
Ajali hiyo imetokea leo jioni katika barabara kuu ya Moshi–Same, ambapo basi la Chanel One lililokuwa likitokea Moshi kuelekea Tanga, liligongana uso kwa uso na Coaster iliyokuwa ikitokea Same kuelekea Moshi.
Taarifa kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa abiria waliokuwemo kwenye Coaster walikuwa wakielekea katika sherehe ya harusi iliyopangwa kufanyika katika ukumbi wa Kuringe Hall, uliopo mjini Moshi.
Jeshi la Polisi na vyombo vya usalama vinaendelea kuchunguza chanzo cha ajali hiyo huku miili ya marehemu ikiendelea kuondolewa kutoka eneo la tukio.
RAIS MWINYI ATEMBELEA BANDA LA NISHATI MAONESHO YA SABASABA
REA YAJIZATITI KUFIKISHA LENGO LA TAIFA KWENYE NISHATI SAFI YA KUPIKIA
CPA KASORE ASISITIZA UMUHIMU WA KUFUNDISHA MAFUNZO YA UFUNDI STADI KWA WATOTO ILI WAWEZE KUJITEGEMEA
TPDC YAJIVUNIA MAFANIKIO YAPATA TUZO SABASABA.
TANESCO YATOA MAJIKO YA UMEME KWA WANANCHI SABASABA.
Maiko Salali achukua fomu ya ubunge Jimbo la Mpwapwa
SERIKALI IMEPUNGUZA TOZO KATIKA ZAO LA KAHAWA KUTOKA 17 HADI 5.
Mkoa wa Katavi umeendelea kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM)
UDOM KUJA NA TEKNOLOJIA MPYA YA KUUZA VIMIMINIKA.
AMANZI NA BABU TALE USO KWA USO JIMBONI