PURA MBIONI KUCHIMBA VISIMA VITATU VYA GESI ASILIA MKOANI MTWARA. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Nishati

PURA MBIONI KUCHIMBA VISIMA VITATU VYA GESI ASILIA MKOANI MTWARA.

MAMLAKA ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli(PURA), imesema kwa sasa ipo kwenye mchakato wa kuchimba visima vitatu vya gesi asilia mkoani Mtwara ambapo ushiriki wa kampuni za kitanzania Shirika la Maendeleo ya Petrol na Gesi (TPDC) itashiriki kwa asilimia 40.

Sophia kingimali
By Sophia kingimali
10 Jul 2025
PURA MBIONI KUCHIMBA VISIMA VITATU VYA GESI ASILIA MKOANI MTWARA.

MAMLAKA ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli(PURA), imesema kwa sasa ipo kwenye mchakato wa kuchimba visima vitatu vya gesi asilia mkoani Mtwara ambapo ushiriki wa kampuni za kitanzania Shirika la Maendeleo ya Petrol na Gesi (TPDC) itashiriki kwa asilimia 40.

Mkurugenzi Mkuu wa PURA, Mhandisi Charles Sangwene amebainisha hayo leo, Julai 9, 2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kutembelea mabanda yaliyopo katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba).

“Uchimbaji wa visima hivyo unaotarajiwa kuanza Novemba 2025 unalenga kuongeza uzalishaji wa gesi asilia kutoka Kitalu cha Mnazi Bay kwa zaidi ya fuli za ujazo milioni 30 kwa siku na tutahakikisha shughuli zote ambazo zinazoweza kutekelezwa na kampuni Tanzania zitafanywa na Watanzania wenyewe,” amesema.

Aidha aliishukuru Serikali kuwa na mwamko wa ushiriki wa watanzania kwenye nafasi hizo za kazi kutokana na kuajiri watumishi kwenye nafasi kutekeleza hayo majukumu.

Ameongeza kuwa kwenye suala la ajira, Serikali imefanya juhudi za makusudi kupitia vyuo vyetu vikuu vimekuja na gani mbalimbali ambazo wanapohitinu inakua rahisi kuwatumia katika kupata ajira,

Pia amefafanua kuwa shughuli za uzalishaji kwenye Mkondo wa Juu wa Petroli kwa upande wa ajira na kampuni umeongezeka kutoka asilimia 55 hadi 85 na kuwa sehemu ya kujivunia.

Kuhusu maonesho hayo, Mhandisi Sangweni amesema kwamba mwaka huu kumekuwa na maboresho makubwa ukilinganisha na miaka ya nyuma kwa kwenda kwani kwa hiki yanakuwa ya kidigitali.

Amesema pia wananchi wamekuwa wengi na kutembelea kujua masuala mbalimbali yanayohusu mafuta na gesi na wanapifika katika banda hilo wamekuwa na maswali mengi kuhusu matumizi ya nishati safi na wamekuwa wakijibiwa vizuri na kutosheka.

TANZANIA  INA UMEME WA KUTOSHA – DKT. BITEKO

TANZANIA INA UMEME WA KUTOSHA – DKT. BITEKO

RAIS MWINYI ATEMBELEA BANDA LA NISHATI MAONESHO YA SABASABA

RAIS MWINYI ATEMBELEA BANDA LA NISHATI MAONESHO YA SABASABA

Wenye malori watakiwa kuweka vifaa vya usalama

Wenye malori watakiwa kuweka vifaa vya usalama

REA Yashukuru Maono ya Rais Samia, Yajipanga Kusambaza Umeme na Nishati Safi Hadi Vitongojini

REA Yashukuru Maono ya Rais Samia, Yajipanga Kusambaza Umeme na Nishati Safi Hadi Vitongojini

EWURA YABORESHA UPATIKANAJI WA HUDUMA KWENYE MITANDAO YAO YA KIJAMII

EWURA YABORESHA UPATIKANAJI WA HUDUMA KWENYE MITANDAO YAO YA KIJAMII