SINGIDA YANG'ARA SEKTA YA UTALII. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Utalii

SINGIDA YANG'ARA SEKTA YA UTALII.

Mkoa wa Singida una mapori tengefu 3 –Rungwa, Muhesi na Kizigo yenye wanyama wa aina mbalimbali wa kuvutia ambapo mbali na mapori hayo mkoa umebarikiwa kuwa na vivutio vingi vya utalii vya kihistoria na asili.

Moreen Rojas
By Moreen Rojas
04 Jul 2025
SINGIDA YANG'ARA SEKTA YA UTALII.

Mkoa una machifu na shughuli zao mbalimbali zilizobeba historia 
nzuri ya maisha ya koo zao zinazovutia watalii wa ndani na nje.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe.Halima Dendego wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuelezea mafanikio ya Serikali ya awamu ya Sita tarehe 04 Julai katika Ofisi za Idara ya Habari - MAELEZO, Dodoma

Aidha amesema Eneo la maji moto la Msule na Sambaru nalo limeendelea kuvutia 
watalii wengi bila kusahau kaburi la shujaa mwanamama Liti na 
mengine mengi.

"Mwanamama huyu ni shujaa kwani alikuwa akitumia nyuki pekee kupigana vita na wakoloni, nyuki hao walikuwa wakiwashambulia tu wakoloni na wala sio watanzania hivyo alijizolea umaarufu Kwa mbinu yake hiyo mpaka umauti ulipomfika"

Aidha amesema kuwa wamekuwa wazalishaji wakubwa wa nyuki kwani wanakijiji cha nyuki ambapo pia hivi Sasa Singida imejizolea umaarufu kupitia Vumbi la Singida ambapo virutubisho 99 vinapatikana kwa wakati  mmoja kwenye Vumbi hilo.

"Nawasihi watanzania wenzangu kuhakikisha mnajipatia Vumbi la Singida kwani lina faida nyingi kwenye miili yetu hivyo litatusaidia katika kinga ya mwili"

Aidha Kwa upande wa Kuku Singida imeendelea kuwa mzalishaji Bora kwenye eneo hilo kwa kuhakikisha wanaendelea kuzalisha Kuku wakubwa wa kienyeji wenye ubora wa hali ya juu.

"Kama mnavyojua kwenye upande wa uzalishaji wa Kuku tuko vizuri na Uongozi unaangalia namna Bora ya kuhakikisha tunaandaa sehemu nzurii ya machinjio Kwa wananchi wetu ili kukuza Biashara hii ya Kuku ndani na nje ya nchi"

Aidha kwenye Sekta ya Sanaa na Michezo Singida Black Stars imekuwa chanzo kikubwa Cha mapato kwani Kila ikicheza wananchi wanapata fedha kupitia nyumba za wageni,vyakula pamoja na usafiri

"Kama mnavyojua Singida hivi Sasa kwenye ligi kuu tuko vizuri na tumemaliza ligi tukiwa nafasi ya Nne hivyo hii ni ishara kwamba timu zingine kama Simba na Yanga zijipange kwani tunakuja Kwa kasi ya ajabu"

"Viwanja 10 vimejengwa,
Ukarabati wa viwanja 6,
joggin clubs 5 zimeundwa,Vituo 12 vya michezo vimeanzishwa,
Shule 5 zinafundisha somo la michezo,
Vikundi 7 vya Sanaa na wasanii 3 wamesajiliwa 
bila kusahau Mkoa umetoa wachezaji kitaifa na kimataifa"

Amesema katika sekta ya afya, mkoa umeongeza idadi ya vituo vya kutolea huduma kutoka 203 mwaka 2020/21 hadi 302 mwaka 2024/25. Kati ya vituo hivyo, zahanati zimeongezeka kutoka 173 hadi 246 na vituo vya afya kutoka 25 hadi 42.

Aidha, hospitali mpya za wilaya tano zimejengwa huku hospitali tatu zikifanyiwa ukarabati mkubwa. Majengo ya huduma za dharura manne na huduma za wagonjwa mahututi matatu yamekamilika, sambamba na vituo vitatu vilivyoboreshwa kwa ajili ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko.

"Kuna mitambo miwili ya kuzalisha hewa ya tiba aina ya oxygen imewekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Manyoni na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mandewa, hatua iliyoongeza uwezo wa kutoa huduma za dharura kwa wagonjwa mahututi," Amesema .

" Jumla ya watoa huduma wa afya wamefikia 2,748, ambapo ajira mpya 634 zimetolewa na watoa huduma 193 wamepelekwa mafunzoni kuongeza ujuzi,".

Ameeleza  kuwa Wastani wa upatikanaji wa dawa umefikia asilimia 93 huku utoaji wa chanjo ukifikia asilimia 102. Huduma za kibingwa, zikiwemo tembezi na za kudumu, zinaendelea kutolewa kwa wananchi katika maeneo mbalimbali ya mkoa.
 

TANZANIA YAENDELEA KUTANGAZA NA KUKUZA KISWAHILI NA UTAMADUNI WAKE KIMATAIFA

TANZANIA YAENDELEA KUTANGAZA NA KUKUZA KISWAHILI NA UTAMADUNI WAKE KIMATAIFA

Mazingira Wezeshi ya Serikali Yafungua Fursa Mpya za Uwekezaji Kupitia TAWA

Mazingira Wezeshi ya Serikali Yafungua Fursa Mpya za Uwekezaji Kupitia TAWA

USHIRIKI WA TAWA KATIKA MAONESHO YA 49 YA BIASHARA YA KIMATAIFA

USHIRIKI WA TAWA KATIKA MAONESHO YA 49 YA BIASHARA YA KIMATAIFA

DKT ABASI AHAMASISHA WATANZANIA KUTEMBELEA TABORA ZOO.

DKT ABASI AHAMASISHA WATANZANIA KUTEMBELEA TABORA ZOO.

MAONESHO YA UTALII NA UWEKEZAJI ZANZIBAR; FURSA  KWA WANANCHI KUJUA VIVUTIO VYA UTALII VILIVYOPO NGORONGORO

MAONESHO YA UTALII NA UWEKEZAJI ZANZIBAR; FURSA KWA WANANCHI KUJUA VIVUTIO VYA UTALII VILIVYOPO NGORONGORO