IDADI YA WATALII WA NDANI WALIOTEMBELEA MKOA WA TABORA IMEONGEZEKA. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Utalii

IDADI YA WATALII WA NDANI WALIOTEMBELEA MKOA WA TABORA IMEONGEZEKA.

Idadi ya watalii wa ndani waliotembelea Mkoa imeongezeka kutoka watalii 1,283 mwaka 2020 hadi 7,397 mwaka 2025 ambapo Mapato yatokanayo na utalii yameongezeka kutoka shilingi 6,167,860 mwaka 2020 hadi shilingi 26,622,674 mwaka 2025.

Moreen Rojas
By Moreen Rojas
11 Jul 2025
IDADI YA WATALII WA NDANI WALIOTEMBELEA MKOA WA TABORA IMEONGEZEKA.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe.Paulo Matiko Chacha wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya Serikali ya awamu ya Sita tarehe 11 Julai 2025 Katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo jijini Dodoma.

Aidha Viwanda 04 vya kuchakata na kufungasha Asali vimejengwa huku uzalishaji wa Asali umeongezeka kutoka tani 1,868.6 mwaka 2020 hadi tani 2,002.48 kwa mwaka 2025.

"Misitu ya hifadhi ya vijiji imeongezeka kutoka misitu 6 yenye ukubwa wa ekari 11,952.5 mwaka 2020 hadi misitu 37 yenye ukubwa wa ekari 330,780.75 mwaka 2025,Miti takriban 1,500,000 imepandwa ambayo ni asilimia 80 ya lengo la Serikali kwa mwaka"

Aidha Kwa upande wa Sekta ya Elimu Mpango wa Elimu bila malipo kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha sita umeendelea kutekelezwa ambapo fedha za kugharamia mpango huo zimeongezeka kutoka Shilingi 12,835,612,200 mwaka 2020 hadi Shilingi 22,676,904,000 mwaka 2025

Idadi ya shule za msingi zimeongezeka kutoka 819 mwaka 2020 hadi 990 mwaka 2025 na idadi ya shule za sekondari zimeongezeka  kutoka 197 mwaka 2020 hadi 264 mwaka 2025

Idadi ya vyumba vya madarasa ya shule za msingi imeongezeka kutoka madarasa 6,074 mwaka 2020 hadi 8,100 mwaka 2025 na kwa shule za sekondari kutoka madarasa 2,251 mwaka 2020 hadi madarasa 4,047 mwaka 2025,Nyumba za walimu wa shule za msingi na sekondari zimeongezeka kutoka 2,076 mwaka 2020 hadi 2,334 mwaka 2025

Aidha Ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba umeongezeka kutoka Asilimia 69.8 mwaka 2021 hadi Asiilimia 70.8 mwaka 2025, kidato cha nne kutoka Asimia 88.4 mwaka 2020 hadi Asilimia 95 mwaka 2025 na kidato cha sita kutoka Asilimia 99.96 mwaka 2020 hadi Asilimia 100 mwaka 2025 huku Idadi ya walimu walioajiriwa katika ngazi ya elimu ya msingi na sekondari imeongezeka kutoka walimu 10,719 mwaka 2020 hadi walimu 12,354 mwaka 2025.

Mwaka 2020 kulikuwa na Vyuo vya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) 3 katika Wilaya ya Tabora, Urambo na Kaliua mpaka kufikia Aprili, 2025 vyuo vya VETA vimejengwa na idadi yake imefikia 6 katika Wilaya za Igunga, Uyui, Tabora, Nzega, Kaliua na Urambo.

"Hali ya usalama ya Mkoa wa Tabora kwa ujumla ni shwari. Ijapokuwa kuna matukio  machache ya uhalifu lakini mkoa unakabiliana nao ipasavyo,Hivyo matukio hayo machache, hayaathiri shughuli za kila siku za Wananchi na mali zao. Jitihada zinaendelea kufanywa na vyombo vya usalama kwa kushirikisha Wananchi na viongozi wengine katika jamii ili kuwezesha Mkoa wa Tabora kuendelea kuwa katika hali ya utulivu na usalama wakati wote"Amesisitiza Mhe. Chacha

Sanjari na hayo  Serikali imeendelea kutilia mkazo umuhimu wa maendeleo ya wananchi pamoja na ushirikishwaji wa makundi maalum ikiwemo Vijana, Wanawake na Watu Wenye Ulemavu ili kuleta usawa wa kijamii na kiuchumi kwa wote.

Katika kufikia azma hiyo mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na Utoaji wa Mikopo ya 10% kwa Vikundi vya Vijana, Wanawake na watu wenye Ulemavu umeongezeka kwa kipindi cha miaka mitano ambapo kuanzia mwaka 2020/21 hadi 2024/25 jumla ya Shilingi bilioni 16.1 zimetolewa kwa vikundi 1,967.

Pamoja na Mpango wa kunusuru kaya masikini unaendelea kutekelezwa ambapo jumla ya Shilingi bilioni 66.17 zilihawilishwa kwa kaya maskini 41,024, katika kipindi husika na miradi ya miundombinu 1,400 ya Elimu, Afya na Barabara imetekelezwa pamoja na kuwezesha walengwa kujiongezea kipato kupitia ufugaji na kilimo.

Aidha Uchumi wa Mkoa unategemea kilimo, ufugaji, uchimbaji madini, uvunaji mazao ya maliasili, biashara, uzalishaji katika viwanda vidogo miundombinu, huduma za jamii na Utawala. Kilimo na Ufugaji huchangia asilimia 70 ya pato la Mkoa ambapo mazao makuu yalimwayo kwa ajili ya chakula ni Mahindi, Mpunga, Mtama, Muhogo, Viazi vitamu, Uwele na jamii ya mikunde. Aidha, mazao ya biashara ni tumbaku, pamba, alizeti, karanga na mchikichi.

"Hali ya Uchumi ya Mkoa wa Tabora imeendelea kuimarika ambapo Pato halisi la Mkoa limekua kutoka Shilingi Trilioni 5.4 mwaka 2020 hadi Shilingi Trilioni 6.3 mwaka 2024 sawa na ukuaji wa asilimia 17. Vilevile, pato la mtu mmoja mmoja limeongezeka kutoka shilingi milioni 1.77 mwaka 2020 hadi shilingi milioni 1.85 mwaka 2024 sawa na ongezeko la asilimia 4.5"

Aidha Serikali imeendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma ya Maji katika Mkoa wa Tabora ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa kaya nyingi zaidi zinaunganishwa na huduma ya maji.

TANZANIA YAENDELEA KUTANGAZA NA KUKUZA KISWAHILI NA UTAMADUNI WAKE KIMATAIFA

TANZANIA YAENDELEA KUTANGAZA NA KUKUZA KISWAHILI NA UTAMADUNI WAKE KIMATAIFA

Mazingira Wezeshi ya Serikali Yafungua Fursa Mpya za Uwekezaji Kupitia TAWA

Mazingira Wezeshi ya Serikali Yafungua Fursa Mpya za Uwekezaji Kupitia TAWA

USHIRIKI WA TAWA KATIKA MAONESHO YA 49 YA BIASHARA YA KIMATAIFA

USHIRIKI WA TAWA KATIKA MAONESHO YA 49 YA BIASHARA YA KIMATAIFA

DKT ABASI AHAMASISHA WATANZANIA KUTEMBELEA TABORA ZOO.

DKT ABASI AHAMASISHA WATANZANIA KUTEMBELEA TABORA ZOO.