EWURA YABORESHA UPATIKANAJI WA HUDUMA KWENYE MITANDAO YAO YA KIJAMII | The Dodoma Post
The Dodoma Post Nishati

EWURA YABORESHA UPATIKANAJI WA HUDUMA KWENYE MITANDAO YAO YA KIJAMII

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji(EWURA) wamesema wateja wao wa leseni hawahitaji kufika ofisini ili kupata huduma Bali huduma zao zote zinapatikana kwenye mitandao yao ,kwa hiyo wamepunguza usumbufu kwa wananchi kwasababu huduma ambazo walikuwa wanazifuata kwenye ofisi zao za Kanda sita hapa nchini ,sasa wanazipata kupitia mifumo ya kidigitali na ni nia yao kwamba wanaendelea kuboresha mifumo ili kuimarisha utoaji wa huduma.

Moreen Rojas, Dodoma
By Moreen Rojas, Dodoma
17 Jun 2025
EWURA YABORESHA UPATIKANAJI WA HUDUMA KWENYE MITANDAO YAO YA KIJAMII

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Dkt.James Andilile wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Amesema kama sehemu ya kuchochea uwajibikaji kwa taasisi wanazosimamia ,wamezitaka kuingia mikataba ya huduma kwa wateja na kwa sababu mara nyingi unaweza kukuta watoaji wa huduma hawatoi taarifa kwa wakati,wamewaelekeza kuhakikisha kwamba wanaweka taarifa kwenye website zao kama  mikataba ya huduma kwa wateja


"Kama wewe unahusika na masuala ya maji ,weka taarifa kwenye website yako ili mwananchi akaangalie na kujua haki  na wajibu wake katika nupatikanaji wa huduma.


'Kwa hiyo sisi kama sehemu moja ya taasisi za Serikali na kama watumishi wa Umma tunaendelea kusisitiza na kuhakikisha kwamba tunatoka huduma katika viwango vya ubora vinavyokubalika ili hatimaye nchi yetu na mama yetu Tanzania aweze kupiga hatua za kiuchumi na kijamii na watu wetu waweze kufurahia matunda ya Serikali yao iliyopo madarakani Wao kama Mamlaka ,wanahusika na masuala ya mafuta,maji, umeme na gesi asili katika masuala ya Udhibiti 

Kama sehemu ya utekelezaji wa matatizo ya Serikali wanajibidisha katika kuhakikisha kwamba huduma zinapatikana katika viwango vinavyotakiwa kwa wananchi wanaowahudumia.

Kama mmavyofahamu huduma ambazo EWURA inazisimamia zinahusu maisha ya watu,unapoongelea maji,mafuta,unaongelea maisha ya watu."Kwa hiyo kama sehemu ya kuboresha utoaji wa huduma katika ushiriki wetu mahali hapa moja  ni kuhudumia wananchi kutokea hapa"

"Hapa ninapoongea tuna mifumo yetu yote ambayo tunaitumia katika kufanya maamuzi ambapo wananchi wanaofika katika banda letu eneo la chinangali park yanapofanyika maonesho haya wanaweza kuhudumiwa

Aidha amesema hivi karibuni wameboresha mifumo yao ya utoaji huduma ili kuendana na kaulimbiu ya Serikali ya kwamba tuende katika mifumo ya kidigitali ili kuimarisha uwajibikaji 

Aidha Bei ya mafuta ni sh 2905  lakini baadhi wanaouza Petroli, baadhi ya vituo wanasema wanauza kuanzia mafuta ya sh 5000Tofauti na hapo ni kinyume na sheria na atakayethibitika atachukuliwa hatua kali ikiwemo kufungiwa kituo chake.Wanaokumbwa na madhara hayo wapinge simu ya bure 0800110030 ili kutoa taarifa maana huo ni ukiukwaji wa sheria Bei iliyotangazwa ni sh 2905 na kama yupo anayeuza kwa zaidi ya bei iliyotangazwa ni kinyume cha sheria.

EWURA ni moja kati ya Mamlaka za Serikali zinazoshiriki maadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma 2025 ikiwa ni sehemu ya taasisi za Serikali zinazolenga kuboresha huduma wanazozitoa kwa wateja wao.

REA Yashukuru Maono ya Rais Samia, Yajipanga Kusambaza Umeme na Nishati Safi Hadi Vitongojini

REA Yashukuru Maono ya Rais Samia, Yajipanga Kusambaza Umeme na Nishati Safi Hadi Vitongojini

NISHATI YA GESI ASILIA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA NCHI.

NISHATI YA GESI ASILIA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA NCHI.

DKT. BITEKO AZINDUA MKAKATI WA TAIFA WA MAWASILIANO WA NISHATI SAFI YA KUPIKIA.

DKT. BITEKO AZINDUA MKAKATI WA TAIFA WA MAWASILIANO WA NISHATI SAFI YA KUPIKIA.

Morocco wampongeza Rais Samia kwa usimamizi bora Sekta ya Nishati

Morocco wampongeza Rais Samia kwa usimamizi bora Sekta ya Nishati

Watu Wenye Ulemavu Waomba Kuangaliwa kwa Jicho la Kipekee Katika Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote.

Watu Wenye Ulemavu Waomba Kuangaliwa kwa Jicho la Kipekee Katika Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote.