DKT ABASI AHAMASISHA WATANZANIA KUTEMBELEA TABORA ZOO. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Utalii

DKT ABASI AHAMASISHA WATANZANIA KUTEMBELEA TABORA ZOO.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, Juni 23, 2025 alifanya ziara katika bustani ya wanyamapori ya Tabora, maarufu kama Tabora ZOO, kwa lengo la kukagua na kuona usimamizi wa bustani hiyo ambapo alitumia fursa hiyo kuwahamasisha Watanzania hususani wa ukanda wa magharibi, wakazi wa Mkoa wa Tabora na Mikoa ya jirani kutembelea kivutio hicho cha kipekee ambacho kipo Katikati ya Mkoa wa Tabora.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
24 Jun 2025
DKT ABASI AHAMASISHA WATANZANIA KUTEMBELEA TABORA ZOO.

* Aahidi Maboresho Makubwa Zaidi ya Miundombinu.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, Juni 23, 2025 alifanya ziara katika bustani ya wanyamapori ya Tabora, maarufu kama Tabora ZOO, kwa lengo la kukagua na kuona usimamizi wa bustani hiyo ambapo alitumia fursa hiyo kuwahamasisha Watanzania hususani wa ukanda wa magharibi, wakazi wa Mkoa wa Tabora na Mikoa ya jirani kutembelea kivutio hicho cha kipekee ambacho kipo Katikati ya Mkoa wa Tabora.

Katika ziara hiyo, Dkt. Abbasi ameonesha kuridhishwa na uwepo wa bustani hiyo ambayo ni hazina ya vivutio vya wanyamapori na mazingira asilia. Ameeleza kuwa Tabora ZOO ni sehemu muhimu ya utalii wa ndani ambayo Serikali imejipanga kuhakikisha inafanya maboresho makubwa ya miundombinu ili kuvutia watalii wengi zaidi.

"Hii ni Hifadhi ya kipekee, kuwa na eneo la heka zaidi ya 27 Katikati ya Manispaa ya Tabora au mji ni jambo kubwa, kwahiyo niwaombe wakazi wa Tabora, hii ni Johari yenu, ni bustani iliyowekwa Kwa ajili yenu mje kupumzika, kujifunza lakini si tu wakazi wa Tabora bali pia wanafunzi wa vyuo mbalimbali na watu wa ukanda huu tunawakaribisha sana," alisema Dkt. Abbasi.

Aidha, Katibu Mkuu huyo ameahidi kuwa Serikali itaendelea kuboresha bustani hiyo kwa kuongeza miundombinu  ikiwemo sehemu za watalii  kupumzika na burudani kama michezo ya watoto,  maeneo ya chakula, vinywaji pamoja na kuongeza Idadi ya wanyamapori  na mabwawa ya maji  ili kuongeza mvuto zaidi kwa watalii.

Katika ziara hiyo Dkt. Abbasi aliweza kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA kupitia bustani hiyo ya wanyamapori na maendelezo yaliyofanyika ikiwemo ujenzi wa kituo cha maelezo Kwa wageni (VIC,), mabanda ya wanyamapori, ongezeko la wanyamapori wakiwemo simba, chui, duma, fisi na wengine wa aina mbalimbali.

Tabora ZOO ambayo ni mojawapo ya bustani chache za wanyamapori  nchini zilizopo katika maeneo ya miji imeendelea kuwa  kivutio cha kipekee Kwa watalii kutokana na  mandhari nzuri na mazingira tulivu ambavyo vinaiweka bustani hii katika nafasi ya juu Kwa utalii wa mijini (Urban Wildlife Tourism).

IDADI YA WATALII WA NDANI WALIOTEMBELEA MKOA WA TABORA IMEONGEZEKA.

IDADI YA WATALII WA NDANI WALIOTEMBELEA MKOA WA TABORA IMEONGEZEKA.

TANZANIA YAENDELEA KUTANGAZA NA KUKUZA KISWAHILI NA UTAMADUNI WAKE KIMATAIFA

TANZANIA YAENDELEA KUTANGAZA NA KUKUZA KISWAHILI NA UTAMADUNI WAKE KIMATAIFA

Mazingira Wezeshi ya Serikali Yafungua Fursa Mpya za Uwekezaji Kupitia TAWA

Mazingira Wezeshi ya Serikali Yafungua Fursa Mpya za Uwekezaji Kupitia TAWA

USHIRIKI WA TAWA KATIKA MAONESHO YA 49 YA BIASHARA YA KIMATAIFA

USHIRIKI WA TAWA KATIKA MAONESHO YA 49 YA BIASHARA YA KIMATAIFA