

Fursa za Uwekezaji zinazopatikana katika maeneo mbalimbali yaliyo chini ya usimamizi wa TAWA, ikiwa ni pamoja na:Makuyuni Wildlife Park (Arusha),Pande (Dar es Salaam),Wami-Mbiki (Morogoro na Pwani),Tabora Zoo (Tabora),Ruhila Zoo (Ruvuma) na mengine mengi
* Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) inashiriki katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa kwa mwaka 2025 yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius K. Nyerere, vilivyopo barabara ya Kilwa, Jijini Dar es Salaam.
* Kupitia maonesho haya, TAWA inatumia fursa hii kutangaza bidhaa na huduma mbalimbali zinazohusiana na utalii na uhifadhi zinazotolewa na Mamlaka hiyo.
*Unapotembelea banda la Wizara ya Maliasili na Utalii, utakutana na maofisa wa TAWA ambao watakupa maelezo kuhusu mambo yafuatayo:
1. Fursa za Uwekezaji zinazopatikana katika maeneo mbalimbali yaliyo chini ya usimamizi wa TAWA, ikiwa ni pamoja na:Makuyuni Wildlife Park (Arusha),Pande (Dar es Salaam),Wami-Mbiki (Morogoro na Pwani),Tabora Zoo (Tabora),Ruhila Zoo (Ruvuma) na mengine mengi
2. Fursa ya Kujionea Wanyamapori Hai kupitia bustani ya wanyamapori iliyopo ndani ya banda la Wizara ya Maliasili na Utalii, kwa viingilio vya bei nafuu kwa Watanzania.
3. Vivutio vya Utalii vilivyopo katika maeneo mbalimbali yanayosimamiwa na TAWA, pamoja na taarifa za gharama na namna ya kuyatembelea.
4. OFA Maalum ya Ziara ya kutembelea Hifadhi ya Pande, iliyopo Jijini Dar es Salaam, kwa gharama nafuu katika msimu huu wa Maonesho ya Sabasaba.
5. Shughuli za Utalii na Uhifadhi zinazofanywa na TAWA, ikiwa ni pamoja na elimu kwa umma kuhusu namna ya kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu, na kuelewa tabia zao.
6. Fursa ya Kufurahia Nyamapori Choma iliyoandaliwa kwa umahiri na kwa kuzingatia ubora wa hali ya juu Kwa bei ya kizalendo.
Karibuni kwa wingi katika banda la Wizara ya Maliasili na Utalii, mjifunze, muelimike na mjionee huduma na vivutio vya kipekee, hasa wanyamapori hai waliopo ndani ya banda hilo.
IDADI YA WATALII WA NDANI WALIOTEMBELEA MKOA WA TABORA IMEONGEZEKA.
DK.NDUMBARO AIPONGEZA OFISI YA MWANDISHI MKUU WA SHERIA.
DKT. YONAZI AONGOZA KIKAO CHA TANZANIA NATIONAL COORDINATING MECHANISM (TNCM)
TANZANIA INA UMEME WA KUTOSHA – DKT. BITEKO
MAMA JANETH MAGUFULI ATEMBELEA BANDA LA OFISI YA WAZIRI MKUU SABASABA*
UDOM KUJA NA TEKNOLOJIA MPYA YA KUUZA VIMIMINIKA.
Mkoa wa Katavi umeendelea kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM)
SINGIDA YANG'ARA SEKTA YA UTALII.
TANZANIA YAENDELEA KUTANGAZA NA KUKUZA KISWAHILI NA UTAMADUNI WAKE KIMATAIFA
OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA KUTOA ELIMU YA SHERIA ZA UCHAGUZI SABASABA.