DCEA YABAINI NJIA MPYA INAYOTUMIWA NA WAFANYABIASHARA WA DAWA ZA KULEVYA KUSAFIRISHIA DAWA HIZO. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

DCEA YABAINI NJIA MPYA INAYOTUMIWA NA WAFANYABIASHARA WA DAWA ZA KULEVYA KUSAFIRISHIA DAWA HIZO.

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya(DCEA), imebaini mbinu mpya inayotumiwa na wauza dawa za kulevya nchini kutumia maiti za binadamu kubebea dawa hizo maarufu kama kibegi.

Sophia Kingimali
By Sophia Kingimali
09 Jul 2025
DCEA YABAINI NJIA MPYA INAYOTUMIWA NA WAFANYABIASHARA WA DAWA ZA KULEVYA  KUSAFIRISHIA DAWA HIZO.

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya(DCEA), imebaini mbinu mpya inayotumiwa na wauza dawa za kulevya nchini kutumia maiti za binadamu kubebea dawa hizo maarufu kama kibegi.

Pia,imewakamata watu wawili wamiliki wa kiwanda bubu kinachotengeneza biskuti zinazochanganywa na bangi kisha kuzisambaza katika mikoa ya Dar es salaam, Mwanza, Lindi na Mtwara.

Haya yamebainishwa leo Julai 9,2025 jijini Dar es Salaam na Kamishna wa Mamlaka hiyo, Aretas Lyimo wakati akizungumzia na waandishi wa habari kuhusu shehena ya dawa mpya zilizokamatwa.

Sambamba na hayk amesema mkoani Lindi alikamatwa mfanyabiashara wa madini akisambaza biskuti zilizochanganywa na bangi.

Amesema katika kipindi cha Mei hadi Julai, 2025, Mamlaka hiyo  kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola, imefanya operesheni katika maeneo mbalimbali nchini na kukamata dawa za kulevya jumla ya kilogramu 37.197.142.

"Mamlaka imebaini kuwa, baadhi ya wahalifu wa dawa za kulevya wameanza tena kutumia maiti za binadamu kubeba dawa za kulevya, maarufu kwa jina la begi. Aidha, kumekuwa na matukio ya raia wa kigeni kuwatumia watanzania kusafirisha au kusambaza dawa za kulevya.

"Mara nyingi, huanzisha mahusiano ya kirafiki na kisha kuwahusisha katika biashara hii haramu kwa kutumia kampuni zao na vyombo vyao vya usafiri hususani bodaboda, bajaji, Tax na wasambazaji wa vifurushi,"amesema.

"Dawa hizo zinajumuisha, kilogramu 11,031.42 za dawa mpya za kulevya (New Psychoactive Substance) aina ya Mitragyna Speciosa, bangi kilogramu 24,873.56, mirungi kilogramu 1,274.47, skanka kilogramu 13.42, heroin kilogramu 2.21 na methamphetamine gramu 1.42,"alisema.

Amesema ukamataji huo umehusisha dawa tiba zenye asili ya kulevya aina ya ketamine kilogramu 1.92, Fluni-trazepam (rohypnol) vidonge 1000, lita 6 za kemikali bashirifu aina ya hydrochloric acid na uteketezaji wa ekari 1,045.5 za mashamba ya bangi.

Aliongeza kuwa kilogram 26 za dawa za kulevya aina ya heroin, zilizokuwa ziingizwe nchini kutokea nchini Msumbiji zilizuiwa lakini pia Watuhumiwa 64 walikamatwa wakihusishwa na dawa hizo.

Katika operesheni iliyofanyika bandari kavu eneo la Temeke jijini Dar es Salaam, kilogramu 11,031.42 za dawa za kulevya aina ya Mitragyna speciosa zilizoingizwa nchini kutokea nchini Sri Lanka zilikamatwa zikiwa kwenye vifungashio vyenye chapa inayoonesha kuwa ndani yake kuna mbolea.

"Mitragyna speciosa iko katika kundi la dawa mpya za kulevya zinazotokana na mimea inayofahamika kwa jina la "Kratom" mmea huu unakemikali aina ya Mitragynine na 7-Hydroxymitragynine (7-HMG) ambayo inasifa ya vichangamshi (stimulants) na vipumbaza (depresants) vyenye madhara ya kiafya kwa mtumiaji kwani huathiri mfumo wa fahamu na kusababisha uraibu hata kupelekea vifo vya ghafla,"alisema.

Katika operesheni iliyofanyika eneo la Posta jijini Dar es Salaam, amesema watuhumiwa sita, wakiwemo raia wawili wa China wanaofahamika kwa majina ya Chein Bai na Qixian Xin walikamatwa wakisafirisha dawa za kulevya aina ya Methamphetamine gramu 1.42, dawa tiba zenye asili ya kulevya aina ya frunitrazepam (rohypnol) vidonge 1,000 na Ketamine zenye uzito wa Kilogramu 1.92.

Kwa upande wa dawa za kulevya za mashambani, amesema zilikamatwa jumla ya kilogramu 26.191.45 za bangi, mirungi, skanka na kuteketeza akan 1,045.5 za mashamba ya bangi katika mikoa ya Ruvuma, Mbeya, Mara, Kagera, Dodoma, Tabora, Morogoro na Arusha.

Amewataka wananchi kuwa makini na kuchukua tahadhari kubwa hasa pale wanapotumwa au kupokea mizigo kutoka kwa watu wasiowafahamu vyema. Ni muhimu wajiridhishe na mizigo wanayoisafirisha ili kuepuka kujikuta wakihusika katika usafirishaji wa dawa za kulevya.

Amewataka watanzania kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali katika kukabiliana na tatizo la dawa za kulevya kwa kuwafichua watu wanaojihusisha kwa namna yoyote ile na dawa za kulevya ili tatizo la dawa hizo litabaki historia hapa nchini.

"Kwa yoyote atakayejihusisha na uzalishaji, usambazaji na biashara ya dawa za kulevya. hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake,"amesema.

DKT. YONAZI AONGOZA KIKAO CHA TANZANIA NATIONAL COORDINATING MECHANISM (TNCM)

DKT. YONAZI AONGOZA KIKAO CHA TANZANIA NATIONAL COORDINATING MECHANISM (TNCM)

CPA KASORE ASISITIZA UMUHIMU WA KUFUNDISHA MAFUNZO YA UFUNDI STADI KWA WATOTO ILI WAWEZE KUJITEGEMEA

CPA KASORE ASISITIZA UMUHIMU WA KUFUNDISHA MAFUNZO YA UFUNDI STADI KWA WATOTO ILI WAWEZE KUJITEGEMEA

TPDC YAJIVUNIA MAFANIKIO YAPATA TUZO SABASABA.

TPDC YAJIVUNIA MAFANIKIO YAPATA TUZO SABASABA.

TANESCO YATOA MAJIKO YA UMEME KWA WANANCHI SABASABA.

TANESCO YATOA MAJIKO YA UMEME KWA WANANCHI SABASABA.

Waziri Ridhiwani Atoa Wito kwa Vijana Kuchangamkia Fursa Zilizopo.

Waziri Ridhiwani Atoa Wito kwa Vijana Kuchangamkia Fursa Zilizopo.