

Mkurugenzi mkuu Mamlaka ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi (VETA) CPA Anthony Kasore amesema kuwa mfumo wa elimu nchini umeendelea kuboreshwa ili kutoa fursa kwa kila mtoto kupata elimu ya vitendo itakayomuwezesha kujitegemea na kuleta mabadiliko chanya katika jamii
Mkurugenzi mkuu Mamlaka ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi (VETA) CPA Anthony Kasore amesema kuwa mfumo wa elimu nchini umeendelea kuboreshwa ili kutoa fursa kwa kila mtoto kupata elimu ya vitendo itakayomuwezesha kujitegemea na kuleta mabadiliko chanya katika jamii.
Akizungumzia na waandishi wa habari julai 7,2025 wakati alipotembelea banda la VETA kwenye maonesho ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba amesema kuna umuhimu wa kuanzisha watoto wadogo kwenye ujuzi wa maisha mapema ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi na kijamii.
"Watoto wadogo wanapaswa kuanza kujifunza ujuzi mapema ili kuwa na ufanisi katika maisha yao ya baadae kwani itapunguza utegemezi",amesema.
Amesema ni lengo lao kubwa kutoa elimu itakayomsaidia kila mtoto wa kitanzania kupata ajira na kujiajiri na kuweza kushiriki katika kukuza uchumi wa nchi.
"Watoto wanapokuwa na ujuzi wa vitendo wanakuwa na uwezo wa kujiajili au kujitegemea na VETA imatoa mafunzo inayowasaidia wanafunzi kuunda na kuuza lakini pia mbinu za ujasiliamali ili waweze kufanya biashara zao kwa ufanisi",Amesema.
Aidha amesema kuwa VETA imejidhatiti kutoa elimu hiyo ya ujasiliamali ili watoto na vijana waweze kujitengenezea fursa za ajira katika jamii zinazowazunguka.
"Tunajivunia kuona mabadiliko makubwa kwenye mfumo wa elimu nchini sisi VETA kwa kushirikiana na Serikali tutaendelea kuwakeza katika mafunzo ya ujuzi ili kuhakikisha vijana wetu wanakuwa na uwezo wa kujiajiri na kuleta mabadiliko chanya katika jamii",Amesema.
IDADI YA WATALII WA NDANI WALIOTEMBELEA MKOA WA TABORA IMEONGEZEKA.
DK.NDUMBARO AIPONGEZA OFISI YA MWANDISHI MKUU WA SHERIA.
DKT. YONAZI AONGOZA KIKAO CHA TANZANIA NATIONAL COORDINATING MECHANISM (TNCM)
TANZANIA INA UMEME WA KUTOSHA – DKT. BITEKO
MAMA JANETH MAGUFULI ATEMBELEA BANDA LA OFISI YA WAZIRI MKUU SABASABA*
UDOM KUJA NA TEKNOLOJIA MPYA YA KUUZA VIMIMINIKA.
Mkoa wa Katavi umeendelea kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM)
SINGIDA YANG'ARA SEKTA YA UTALII.
TANZANIA YAENDELEA KUTANGAZA NA KUKUZA KISWAHILI NA UTAMADUNI WAKE KIMATAIFA
OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA KUTOA ELIMU YA SHERIA ZA UCHAGUZI SABASABA.