UDSM YASAINI MAKUBALIANO NA KAMPUNI ZA CHINA KUTOA MAFUNZO KWA VITENDO KWA WANAFUNZI WA CHUO HICHO. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

UDSM YASAINI MAKUBALIANO NA KAMPUNI ZA CHINA KUTOA MAFUNZO KWA VITENDO KWA WANAFUNZI WA CHUO HICHO.

Chuo kikuu Cha Dar es salaam kimesaini makubalinao ya ushirikiano na Kampuni mbili za uchina ambao utawezesha wanafunzi wa chuo hicho kupata nafasi ya kufanya mafunzo Kwa vitendo ili kupata ujuzi halisi wa fani wanazosomea.

Sophia Kingimali
By Sophia Kingimali
23 Jun 2025
UDSM YASAINI MAKUBALIANO NA KAMPUNI ZA CHINA KUTOA MAFUNZO KWA VITENDO KWA WANAFUNZI WA CHUO HICHO.

Chuo kikuu Cha Dar es salaam kimesaini makubalinao ya ushirikiano na Kampuni mbili za uchina ambao utawezesha wanafunzi wa chuo hicho kupata nafasi ya kufanya mafunzo Kwa vitendo ili kupata ujuzi halisi wa fani wanazosomea.

Akizungumza leo Juni 23,2025 jijini Dar es Salaam mara baada ya Halfa ya utiaji Saini hati za makubaliano hayo Makamu Mkuu wa chuo kikuu cha Da es salaam (UDSM) Prof William Anangisye amesema mbali na wanafunzi kupata nafasi ya kufanya mafunzo Kwa vitendo katika kampuni hizo lakini pia kampuni hizo  zimekubali kutoa ufadhili wa masomo Kwa wanafunzi wa chuo hicho.

"Hii ni fursa kwetu kama chuo lakini pia kwa nchi yetu kwani wanafunzi wetu watapata fursa ya kupata
mafunzo kwa vitendo hali itakayowapelekea vijana kupata uzoefu kabla ya kuajiliwa lakini pia kampuni hizo zitatoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wetu",Amesema Prof.Anangisye.

Kwa upande wao Watumishi wa kampuni hizo mbili ambao ni Mkurugenzi Mtendaji wa ,JUYE concrete company--Ms  Hongjuan Xu na Mkurugenzi mtendaji wa Let's KZJ group Dr. Xiuxing Ma 3, Let's KZJ Chief engineer--Dr Yunhui Fang ambazo zimeingia makubalino na chuo kikuu Cha Dar es salaam wamesema wataendelea kushirikiana na Tanzania katika kubadilishana ujuzi ikiwemo kiwafundisha wahandisi na mafundi wa Tanzania  kuhusu teknolojia ya kisasa ya zege ambayo imetumika katika ujenzi wa miradi mingi hapa nchini ikiwemo mradi wa daraja la Magufuli na Daraja la Tanzanite.

Katika makubalinao hayo hati ya kwanza itadumu Kwa kipindi Cha miaka mitano na hati nyingine itadumu Kwa kipindi Cha miaka mitatu huku kukiwa na nafasi ya kuhuisha makubalino hayo Kwa faida ya wanafunzi wa chuo hicho.

Waziri Ridhiwani Atoa Wito kwa Vijana Kuchangamkia Fursa Zilizopo.

Waziri Ridhiwani Atoa Wito kwa Vijana Kuchangamkia Fursa Zilizopo.

TPDC ,DC CPP na CPTDC ZASAINI MAKUBALIANO UJENZI WA BOMBA LA GESI ASILIA KUTOKA NTORYA HADI MADIMBA.

TPDC ,DC CPP na CPTDC ZASAINI MAKUBALIANO UJENZI WA BOMBA LA GESI ASILIA KUTOKA NTORYA HADI MADIMBA.

TAKUKURU YAWATAKA VIONGOZI WA DINI KUKEMEA RUSHWA.

TAKUKURU YAWATAKA VIONGOZI WA DINI KUKEMEA RUSHWA.

OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA KUTOA ELIMU YA SHERIA ZA UCHAGUZI SABASABA.

OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA KUTOA ELIMU YA SHERIA ZA UCHAGUZI SABASABA.

Mkoa wa Katavi umeendelea kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM)

Mkoa wa Katavi umeendelea kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM)