

Katika kuhakikisha tunakuza na kudumisha Utamaduni wa Kitanzania katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita,Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, imeratibu jumla ya Matamasha matatu (3) ya Kitaifa ya Utamaduni,ambapo Tamasha la Kwanza la Utamaduni wa Mtanzania lilifanyika mwezi Juni, 2022, jijini Dodoma, Tamasha la Pili lilifanyika mwezi Agosti, 2023, mkoani Njombe, na Tamasha la Tatu lilifanyika mwezi Septemba, 2024, mkoani Ruvuma
Hayo yameelezwa na Prof.Palamagamba kabudi Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo wakati akizungumza na waandishi wa habari Aprili 14 kuelekea maadhimisho ya miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita kuelezea mafanikio na mwelekeo wa Wizara hiyo katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo Dodoma.
Aidha amesema Matamasha haya yamelenga kuonesha na kudumisha tamaduni za makabila ya Tanzania kwa maonesho ya ngoma, sanaa, na michezo ya asili, na pia yamekuwa jukwaa la kuhamasisha wananchi kushiriki katika kuenzi na kudumisha urithi wa utamaduni wa Kitanzania.
Aidha katika kipindi kifupi cha uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita, Serikali imefanikiwa kutambua na kuenzi Kiswahili kama lugha muhimu kimataifa. Hii ni baada ya tarehe 7 Julai kutambuliwa rasmi na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kama Siku ya Kiswahili Duniani.
"Uamuzi huu ulifanyika mnamo tarehe 1 Julai, 2024, katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Marekani. Mafanikio haya yanadhihirisha uongozi thabiti wa Serikali ya Awamu ya Sita katika kukuza na kutangaza Kiswahili katika jukwaa la kimataifa"
Aidha Serikali kupitia Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) imeratibu Kongamano la Kwanza la Kimataifa la Kiswahili, lililofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Havana, nchini Kuba, kuanzia tarehe 07 hadi 10 Novemba 2024, kongamano hili limekuwa hatua muhimu katika kuimarisha Kiswahili kama lugha yenye umaarufu na umuhimu katika majukwaa ya kimataifa, na pia limeongeza utambulisho wa Tanzania duniani kote.
"Pamoja na kongamano hili, BAKITA lilizindua Kamusi ya Kiswahili - Kihispaniola, hatua ambayo imeendelea kukuza na kueneza Kiswahili,Kongamano hilo lilihusisha washiriki takribani 600, likiongozwa na kaulimbiu isemayo: “Ustawi wa Kiswahili Duniani: Tulikotoka, Tulipo na Tunakokwenda.”
Aidha ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita katika kipindi cha miaka minne, imefanikiwa kufungua vituo 19 vya kufundisha Kiswahili kupitia balozi za Tanzania katika nchi za Uholanzi, Abu Dhabi, Italia, Zimbabwe, Nigeria, Uswisi, Ufaransa, na Uturuki. Hii inafanya kuwa na jumla ya vituo 19 vya kufundisha Kiswahili nje ya Tanzania.
"Hatua hii ni muhimu katika kukuza na kueneza Kiswahili duniani kote, na inachangia katika kuongeza umaarufu wa lugha hii katika maeneo mbalimbali ya kimataifa, Ambapo kwa sasa ni miongoni mwa lugha 7 kubwa zaidi Duniani yenye takribani wazungumzaji takribani millioni 500"
"Kwa mapenzi makubwa ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kukuza na kuwaendeleza Wasanii Nchini, katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake amefanikiwa kuhuisha Mfuko wa Utamaduni na Sanaa ambao ulianza kufanya kazi rasmi Desemba 2022. Ambapo katika kipindi hicho mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 5.25 imetolewa kwa miradi 359 ya Utamaduni na Sanaa katika mikoa 19 nchini,hatua hii imepelekea kuongeza ajira kwa vijana na kuongezeka kwa ubora wa kazi za sanaa na burudani"
Sanjari na hayo Serikali ya Awamu ya Sita imefanikiwa kuhuisha na kuendeleza wazo la muda mrefu la ujenzi wa Sports and Arts Arena. Mradi huu wa kisasa, unaotarajiwa kugharimu takribani Shilingi bilioni 300, unatarajiwa kufadhiliwa kupitia mkopo wa masharti nafuu kutoka nchini Korea, na utakapokamilika utakuwa ni moja ya vituo vikubwa vya michezo na sanaa katika Ukanda wa Afrika Mashariki, ukiwa kichocheo cha ajira, burudani, utalii na maendeleo ya vipaji vya vijana.
"Hatua hii inaonesha dhamira ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kuiendeleza sekta ya michezo na sanaa kwa kiwango cha kimataifa, sambamba na kuwekeza kwenye miundombinu yenye tija kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi"
Aidha Idara ya Habari-MAELEZO imeimarishwa kwa kununuliwa vitendea kazi vikiwemo magari na vifaa vya kurushia matangazo mbashara na kuvilisha matangazo hayo vyombo vingine vya habari vya Televusheni na Televisheni Mtandao hata katika katika mkutano huu, MAELEZO ndio wanafanya uzalishaji wa maudhui mbashara na kuvilisha vyombo vyombo vingine vya habari.
PPAA yatoa elimu matumizi ya Moduli Wiki ya Utumishi wa Umma
KIHENZILE: UWAZI NA UWAJIBIKAJI NI NGUZO MUHIMU ZENYE TIJA KWA WANANCHI
KIHENZILE:WIKI YA UTUMISHI WA UMMA NI FURSA MUHIMU KWA WANANCHI
ACT WAZALENDO KUUWASHA MOTO MANZESE WAJIDHATITI KUCHUKUA MAJIMBO YOTE DAR ES SALAAM
TANESCO YAJA NA KAMPENI MAALUM YA KUHAMASISHA ULIPAJI WA MADENI KWA WATEJA.
GRAND BUNGE BONANZA KUFANYIKA JUNI 21 2025 HUKU MGENI RASMI AKITARAJIWA KUWA RAIS SAMIA.
KIHENZILE:WIKI YA UTUMISHI WA UMMA NI FURSA MUHIMU KWA WANANCHI
NISHATI YA GESI ASILIA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA NCHI.
MOI YASEMA WAGONJWA WENGI WANAOWAHUDUMIA WANA MATATIZO SUGU.
CDE SALUM ATANGAZA NIA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAHAMA MJINI.