Jay Z na Familia Yake Wapata Vitisho Kufuatia Kesi ya Ubakaji | The Dodoma Post
The Dodoma Post Burudani

Jay Z na Familia Yake Wapata Vitisho Kufuatia Kesi ya Ubakaji

Rapa maarufu Jay Z na familia yake wanaripotiwa kupokea vitisho vya kuuawa kutoka kwa watu mbalimbali mitandaoni, kufuatia kesi ya ubakaji inayomhusisha binti wa miaka 13, anayedaiwa kubakwa na Diddy mwaka 2000. Kesi hiyo ilifunguliwa na mwanadada aliyejulikana kwa jina bandia la 'Jane Doe' Desemba 9, 2024, akidai kuwa alifanyiwa unyanyasaji baada ya sherehe za tuzo za Video Music Awards (VMAs).

GIlbert ludovick
By GIlbert ludovick
19 Feb 2025
Jay Z na Familia Yake Wapata Vitisho Kufuatia Kesi ya Ubakaji

Jay Z anadai kuwa yeye na familia yake wamekuwa wakituhumiwa kuwa ni waongo na waovu, huku wengine wakitaka apelekwe gerezani kama alivyofanya Diddy na kisha auliwe. Kesi hii, hata hivyo, imeshafutwa baada ya mshitakiwa kuiondoa kwa hiari, na hivyo kuondoa tuhuma hizo kisheria.

Hata hivyo, mjadala unaendelea mitandaoni, huku baadhi ya watu wakidai kuwa haki haikutendeka. Vitisho vinavyotolewa kwa Jay Z na familia yake ni kielelezo cha madhara ya mitandao ya kijamii katika kujenga au kubomoa sifa za watu, hasa katika kesi kubwa kama hii.

Ibraah Afunguka: "Nilifukuzwa Konde Gang na Harmonize"

Ibraah Afunguka: "Nilifukuzwa Konde Gang na Harmonize"

Serikali imeratibu jumla ya matamasha matatu ya Kitaifa ya utamaduni.

Serikali imeratibu jumla ya matamasha matatu ya Kitaifa ya utamaduni.

DrKumbuka Afunguka Kuhusu Kuvunjika kwa Ndoa ya Haji Manara na Zaiylissa

DrKumbuka Afunguka Kuhusu Kuvunjika kwa Ndoa ya Haji Manara na Zaiylissa

WASANII WAPEWA MAFUNZO YA KUGEUZA SANAA KUTOKA KUWA BURUDANI HADI BIASHARA.

WASANII WAPEWA MAFUNZO YA KUGEUZA SANAA KUTOKA KUWA BURUDANI HADI BIASHARA.

"A$AP Rocky Amzuia  rafiki yake Twelvyy Kujibu Maswali Mahakamani"

"A$AP Rocky Amzuia rafiki yake Twelvyy Kujibu Maswali Mahakamani"