

Kesi inayomhusu rapa maarufu A$AP Rocky imeendelea kuibua maswali baada ya tukio la kipekee kutokea mahakamani. Katika kusikiliza kwa kesi ya shambulio mapema jana, A$AP Rocky alijitokeza kumzuia rafiki yake, A$AP Twelvyy, asijibu swali lililoulizwa na mahakama, jambo lililosababisha hali ya kutatanisha.
Waendesha mashtaka walimhoji Twelvyy kuhusu picha ya kitanda cha Rocky kilichoandikwa neno "AWGE", wakitaka kujua maana yake. Kabla Twelvyy hajatoa majibu, Rocky alikurupuka kwa kupaza sauti akisema, "Usiseme!" Hali hiyo ilisababisha hali ya mshikamano, huku Twelvyy akijibu kwa upole, "Inamaanisha AWGE."
Hata hivyo, mwendesha mashtaka alikasirishwa na ukimya wa Twelvyy, na aliiomba mahakama iamulie kumlazimisha kutoa majibu ya moja kwa moja. Hata hivyo, Twelvyy alikataa kusema chochote zaidi kuhusu maana ya herufi hizo nne. Wakili wa A$AP Rocky, Joe Tacopina, alijitokeza kuomba mazungumzo ya faragha na jaji ili kuzuia kuendelea kwa uchunguzi huu.
Mwisho wa siku, Twelvyy alikataa kufichua siri hiyo ya "AWGE", inayodaiwa kuwa ni shirika la ubunifu lilioanzishwa na Rocky mwaka 2014. Kwa mujibu wa taarifa, kanuni kuu ya AWGE ni ‘Kamwe usifichue maana ya AWGE’.
A$AP Rocky, ambaye anahusishwa na mashtaka mawili ya uhalifu, anadaiwa kumshambulia kwa risasi rafiki yake wa zamani na mshirika wa kundi la muziki la ASAP Mob.
PPAA yatoa elimu matumizi ya Moduli Wiki ya Utumishi wa Umma
KIHENZILE: UWAZI NA UWAJIBIKAJI NI NGUZO MUHIMU ZENYE TIJA KWA WANANCHI
KIHENZILE:WIKI YA UTUMISHI WA UMMA NI FURSA MUHIMU KWA WANANCHI
ACT WAZALENDO KUUWASHA MOTO MANZESE WAJIDHATITI KUCHUKUA MAJIMBO YOTE DAR ES SALAAM
TANESCO YAJA NA KAMPENI MAALUM YA KUHAMASISHA ULIPAJI WA MADENI KWA WATEJA.
GRAND BUNGE BONANZA KUFANYIKA JUNI 21 2025 HUKU MGENI RASMI AKITARAJIWA KUWA RAIS SAMIA.
KIHENZILE:WIKI YA UTUMISHI WA UMMA NI FURSA MUHIMU KWA WANANCHI
NISHATI YA GESI ASILIA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA NCHI.
MOI YASEMA WAGONJWA WENGI WANAOWAHUDUMIA WANA MATATIZO SUGU.
CDE SALUM ATANGAZA NIA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAHAMA MJINI.