CDE SALUM ATANGAZA NIA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAHAMA MJINI. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Siasa

CDE SALUM ATANGAZA NIA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAHAMA MJINI.

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa UVCCM seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Dodoma CDE.Salum Ismaili Salum ametangaza Nia ya kugombea ubunge Jimbo la Kahama Mjini Mkoani Shinyanga huku akitoa rai kwa wananchi kumuunga mkono Rais Dkt Samia kutokana na mazuri aliyofanya katika Uongozi wake .

Ngonise Kahise
By Ngonise Kahise
18 Jun 2025
CDE SALUM ATANGAZA NIA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAHAMA MJINI.

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa UVCCM seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Dodoma CDE.Salum Ismaili Salum ametangaza Nia ya kugombea ubunge Jimbo la Kahama Mjini Mkoani Shinyanga huku akitoa rai kwa wananchi kumuunga mkono Rais Dkt Samia kutokana na mazuri aliyofanya katika Uongozi wake .

Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 18,2025 Jijini Dar es Salaam Salum amesema amevutiwa na hamasa inayotolewa na Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt Samia Suluhu Hassan yakuwataka vijana wengi kujitokeza kugombea katika nafasi mbalimbali za uongozi.

"Nimeamua kutagaza nia ya kugombea ni kwa ajili ya kuwaletea maendeleo Wananchi wa Kahama mjini kwani kupitia fursa nyingi zilizopo jimboni humo ikijumuisha madini "amesema

Amesema Juni 28 Mwaka huu atakuwa ni miongoni mwa watakaojitokeza kuchukua fomu. Aidha amesema kutokana na mambo mazuri yaliyofanywa na Rais Dk Samia katika kuliletea Taifa maendeleo wananchi awanabudi kumuunga mkono ili azidi kusukuma maendeleo ya nchi mbele.

"Rais Dkt Samia Wakati anapokea kijiti Cha uongozi baada ya kifo cha Rais Dkt. John Magufuli na miradi mingi ambayo ilikuwa ikiendelea Kutokana na Mazingira haya watu wengi walidhani Rais Samia asingeweza kuiendelea na kuikamilisha, hivyo ameitekeleza vizuri na kuikamilisha jambo ambalo linafanya Watanzania wamuunge mkono"amesema

Aidha amekemea watu wanaomkejeli na kumsema vibaya kwamba hawatawavumilia. Sambamba na hayo amewataka wananchi hasa vijana kuendelea kuilinda amani ya nchi kwa kuepuka kutumika katika kuivunja amani iliyopo nchini.

KIHENZILE: UWAZI NA UWAJIBIKAJI NI NGUZO MUHIMU ZENYE TIJA KWA WANANCHI

KIHENZILE: UWAZI NA UWAJIBIKAJI NI NGUZO MUHIMU ZENYE TIJA KWA WANANCHI

ACT WAZALENDO KUUWASHA MOTO MANZESE WAJIDHATITI KUCHUKUA MAJIMBO YOTE DAR ES SALAAM

ACT WAZALENDO KUUWASHA MOTO MANZESE WAJIDHATITI KUCHUKUA MAJIMBO YOTE DAR ES SALAAM

Serikali Yatangaza Kuanza Msako Kuwabaini Wanaotumikisha Watoto

Serikali Yatangaza Kuanza Msako Kuwabaini Wanaotumikisha Watoto

VIJANA WANAOTUMIA VIBAYA MITANDAO YA KIJAMII WAONYWA.

VIJANA WANAOTUMIA VIBAYA MITANDAO YA KIJAMII WAONYWA.

VIONGOZI WAANZA KUWAOGOPA WAJUMBE MOROGORO.

VIONGOZI WAANZA KUWAOGOPA WAJUMBE MOROGORO.