

Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) imeshiriki maadhimisho ya kitaifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma, yanayojumuisha Wizara, Sekretarieti za Mikoa na Taasisi mbalimbali za Umma kwa lengo la kutoa elimu kwa wadau wa ununuzi nchini na wananchi kwa ujumla.
PPAA imeshiriki maadhimisho hayo yaliyoratibiwa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma kwa lengo la kutoa elimu pamoja na kuonesha uwajibikaji katika utoaji wa huduma kwa wananchi kuhusu shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Mamlaka ya Rufani.
Akiongea kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa PPAA, Bw. James Sando wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma PPAA, Bw. Nelson Kessy amesema kupitia maadhimisho ya Wiki ya Utumishi, PPAA imepata fursa ya kutoa elimu kuhusu matumizi ya moduli ya kupokea na kushughulikia malalamiko na rufaa katika mfumo wa NeST.
“Pamoja na mambo mengine, moduli hii imesaidia kuokoa muda, gharama, kuongeza uwazi na uwajibikaji katika ununuzi wa umma na kutunza kumbukumbu kwa ujumla,” amesema Bw. Kessy
Bw. Kessy ameongeza kuwa PPAA imetumia jitihada mbalimbali za kuwapatia wazabuni mafunzo mahususi kuhusu matumizi ya moduli ya kupokea na kushughulikia malalamiko na rufaa katika mfumo wa NeST inawafikia wadau wa ununuzi wa umma ili kuisaidia Serikali kupata thamani halisi ya fedha.
Moja ya jitihada hizo ni pamoja na kutoa mafunzo kwa wazabuni na wadau wa ununuzi wa umma katika Kanda ya Ziwa, Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na Kanda ya Kati. Aidha, katika mafunzo hayo PPAA ilifanikiwa kutoa elimu kwa wazabuni 873 na wakuu wa Idara/Vitengo vya ununuzi na sheria wapatao 1,588 kutoka katika taasisi nunuzi 500.
Sanjari na mafunzo, PPAA imetumia maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kuelimisha wananchi na wadau wa ununuzi kuhusu matumizi ya Moduli ya kupokea na kushughulikia Malalamiko na rufaa kieletroniki ikiwemo kuokoa muda na gharama.
Maadhimisho ya wiki ya Utumishi ya mwaka 2025 yamezikutanisha pamoja Wizara, Sekretarieti za Mikoa na Taasisi mbalimbali za Umma, kwa lengo la kuonesha uwajibikaji wa taasisi hizo katika utoaji wa huduma na bidhaa kwa wananchi pamoja na kutoa elimu kuhusu shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na taasisi hizo.
Awali akifungua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Utumishi, Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (Mb.) alizisisitiza taasisi za Serikali kuhakikisha kuwa zinatoa kipaumbele kikubwa katika matumizi ya TEHAMA ili kuongeza ufanisi katika kazi na kuboresha utoaji wa huduma kwa umma.
“Napenda kutoa wito kwa taasisi za umma zote kuhakikisha zinatumia TEHAMA vizuri ili wananchi waweze kuendelea kupata huduma bora haraka na kwa urahisi,” alisema Waziri Simbachawene.
Kaulimbiu ya maadhimisho hayo kitaifa ni: "Himiza Matumizi ya Mifumo ya Kidigiti ili kuongeza Upatikanaji wa Taarifa na kuchagiza Uwajibikaji".
Siku ya Utumishi wa Umma Barani Afrika huadhimishwa kila mwaka tarehe 23 Juni na nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU), ikiwa ni ishara ya kutambua mchango muhimu wa watumishi wa umma katika maendeleo ya nchi zao na bara kwa ujumla.
KIHENZILE: UWAZI NA UWAJIBIKAJI NI NGUZO MUHIMU ZENYE TIJA KWA WANANCHI
KIHENZILE:WIKI YA UTUMISHI WA UMMA NI FURSA MUHIMU KWA WANANCHI
ACT WAZALENDO KUUWASHA MOTO MANZESE WAJIDHATITI KUCHUKUA MAJIMBO YOTE DAR ES SALAAM
TANESCO YAJA NA KAMPENI MAALUM YA KUHAMASISHA ULIPAJI WA MADENI KWA WATEJA.
CDE SALUM ATANGAZA NIA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAHAMA MJINI.
DODOMA YAELEKEA IRINGA KWA KISHINDO MASHINDANO YA UMISSETA.
Serikali Yatangaza Kuanza Msako Kuwabaini Wanaotumikisha Watoto
GRAND BUNGE BONANZA KUFANYIKA JUNI 21 2025 HUKU MGENI RASMI AKITARAJIWA KUWA RAIS SAMIA.
MOI YASEMA WAGONJWA WENGI WANAOWAHUDUMIA WANA MATATIZO SUGU.
NISHATI YA GESI ASILIA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA NCHI.