ULINZI NA USALAMA BAHARINI UMEIMARIKA;TASAC | The Dodoma Post
The Dodoma Post Biashara

ULINZI NA USALAMA BAHARINI UMEIMARIKA;TASAC

Mwenyekiti wa bodi Shirika la uwakala wa meli Tanzania(TASAC) Nahodha Mussa Mandia amesema usafiri wa bahari umezidi kuimarika kiulinzi na usalama hali iliyopelekea kuendelea kuchangia katika ukuaji wa uchumi nchini.

Sophia Kingimali.
By Sophia Kingimali.
05 Jul 2025
ULINZI NA USALAMA BAHARINI UMEIMARIKA;TASAC

Mwenyekiti wa bodi Shirika la uwakala wa meli Tanzania(TASAC) Nahodha Mussa Mandia amesema usafiri wa bahari umezidi kuimarika kiulinzi na usalama  hali iliyopelekea kuendelea kuchangia katika ukuaji wa uchumi nchini.

Pia,ametoa rai kwa wananchi kutembelea kwenye banda lao lililopo kwenye maonesho ya sabasaba ili waweze kujifunza namna shirika hilo linavyofanya kazi katika kuhakikisha linalinda usalama katika bahari.

Akizungumza na waandishi wa habari leo julai 5,2025 jijini Dar es salaam kwenye maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba mara baada ya kutembelea banda hilo amesema vitu vingi karibu asilimia 90 vinasafirishwa kwa kutumia bahari.

"TASAC tunajukumu la kuchajiisha watu kushiriki ulinzi na usalama lakini pia usafiri na usafirishaji katika bahari hivyo tupo hapa kwa ajili ya kuelimisha watu kujua ni kiasi gani usafiri wa bahari unachangia katika uchumi wa nchi",Amesema Nahodha Mandia.

Amesema uwepo wa mazingira mazuri katika bahari umepelekea utalii kwa njia ya bahari unakua lakini pia miradi ya mafuta na gesi inaimarika.

"Tunajukumu la kuhakikisha mazingira ya bahari yanatuzwa kwani yasipotuzwa uchumi utaharibika na utalii kwa njia ya bahari pia utaharibika lakini pia miradi ya mafuta na gesi ndani ya bahari itaharibika",amesema.

Ameongeza kuwa usalama wa bahari kwa kiasi kikubwa umeimarika kwani hata matukio ya maharamia yameisha

"Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vinafanyakazi kubwa kuhakikisha usalama katika bahari unaendelea kuimarika hivyo tunavipongeza kwa kazi kubwa wanayoifanya".Ameongeza Nahodha Mandia.

MAMA JANETH MAGUFULI ATEMBELEA BANDA LA OFISI YA WAZIRI MKUU SABASABA*

MAMA JANETH MAGUFULI ATEMBELEA BANDA LA OFISI YA WAZIRI MKUU SABASABA*

eGA Yaonesha Namna Serikali Inavyotekeleza Mageuzi Kidigitali kwenye Maonesho ya sabasaba.

eGA Yaonesha Namna Serikali Inavyotekeleza Mageuzi Kidigitali kwenye Maonesho ya sabasaba.

RAIS MWINYI ATEMBELEA BANDA LA NISHATI MAONESHO YA SABASABA

RAIS MWINYI ATEMBELEA BANDA LA NISHATI MAONESHO YA SABASABA

BODI YA MKONGE TANZANIA YATANGAZA FURSA  KWA WATANZANIA.

BODI YA MKONGE TANZANIA YATANGAZA FURSA KWA WATANZANIA.

DCEA:SERIKALI IMEPUNGUZA KASI YA WALAIBU WA DAWA ZA KULEVYA.

DCEA:SERIKALI IMEPUNGUZA KASI YA WALAIBU WA DAWA ZA KULEVYA.