

Kaimu mkurugenzi mkuu wa tume ya ushindani (FCC) Tanzania bi.Hadija Ngasongwa ametoa rai wa watanzania kujitokeza kwa wingi kwenye banda lao lililopo katika maonesho ya biashara sabasaba ili wapate kujifunza elimu ya ushindani lakini namna bora ya kutambua bidhaa bandia.
Kaimu mkurugenzi mkuu wa tume ya ushindani (FCC) Tanzania bi.Hadija Ngasongwa ametoa rai wa watanzania kujitokeza kwa wingi kwenye banda lao lililopo katika maonesho ya biashara sabasaba ili wapate kujifunza elimu ya ushindani lakini namna bora ya kutambua bidhaa bandia.
Pia amewataka wawekezaji nchini kujitokeza ili kujifunza na kuzijua sheria zinazosimamia uwekezaji nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 4 julai 2025 alipofanya ziara kwenye banda la viwanda na biashara katika maonyesho ya 49 ya biashara sabasaba amesema wawekezaji wa ndani ya nchi wanasimamiwa na sheria madhubuti zinazosimamia uwekezaji nchini, kusaidia kuimarisha biashara nchini.
" sisi tupo hapa kutekeleza kuendeleza na kutimiza azma ya Rais wa jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha hali ya biashara nchini Tanzania " amesema bi. Hadija
Aidha amesistiza lengo la kuanzishwa tume ya ushindani ni kusimamia na kuhimarisha ufanyaji wa biashara nchini, kulinda na kuhimarisha walaji dhidi ya mienendo potofu ya hali ya ufanyaji biashara nchini kati ya kampuni na kampuni, pamoja na kudhibiti bidhaa bandia.
Awali bi. Hadija Juma amesema lengo kubwa ni kuhakikisha uwekezaji ndani ya nchi waone kwamba kunasheria madhubuti ambazo zitawalinda na kusimamia uwekezaji wao wanaofanya.
" Tunajivunia na tunashukuru sana serikali kuweza kutengeneza mazingira sahihi ya wawekezaji kuhakikisha kwamba mwekezaji wa ndani kuweza kupata fursa zinazopatikana na ufanyaji wa biashara na mazingira mazuri yaliyowekwa katika serikali yetu" amesema Hadija
Pia ameongezea wameweza kushiriki katika maonyesho ya sabasaba ni fahari kwao na kuwaomba wageni wanaopita kwenye maonyesho kuchukua fursa zaidi ya makampuni 3000 yanayopatikana kwenye banda la viwanda na biashara.
Mwenye mtaji mdogo anaweza kupata fursa kuungana na mwenye kipato kikubwa au mwenye uwekezaji mkubwa na kuweza kuhimarisha biashara
Aidha amesistiza kuna sheria ambayo ya kudhibiti bidhaa bandia, ni kosa la jinai kujihusisha na bidhaa bandia hivyo wananchi wafike kwenye banda la viwanda na biashara ili waweze kutofautisha bidhaa bandia na halisi kwa sababu kuna wataalamu wanatoa elimu.
IDADI YA WATALII WA NDANI WALIOTEMBELEA MKOA WA TABORA IMEONGEZEKA.
DK.NDUMBARO AIPONGEZA OFISI YA MWANDISHI MKUU WA SHERIA.
DKT. YONAZI AONGOZA KIKAO CHA TANZANIA NATIONAL COORDINATING MECHANISM (TNCM)
TANZANIA INA UMEME WA KUTOSHA – DKT. BITEKO
MAMA JANETH MAGUFULI ATEMBELEA BANDA LA OFISI YA WAZIRI MKUU SABASABA*
UDOM KUJA NA TEKNOLOJIA MPYA YA KUUZA VIMIMINIKA.
Mkoa wa Katavi umeendelea kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM)
TANZANIA YAENDELEA KUTANGAZA NA KUKUZA KISWAHILI NA UTAMADUNI WAKE KIMATAIFA
SINGIDA YANG'ARA SEKTA YA UTALII.
OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA KUTOA ELIMU YA SHERIA ZA UCHAGUZI SABASABA.