FCC YATOA ELIMU YA UTAMBUZI BIDHAA FEKI SABASABA. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Biashara

FCC YATOA ELIMU YA UTAMBUZI BIDHAA FEKI SABASABA.

Kaimu mkurugenzi mkuu wa tume ya ushindani (FCC) Tanzania bi.Hadija Ngasongwa ametoa rai wa watanzania kujitokeza kwa wingi kwenye banda lao lililopo katika maonesho ya biashara sabasaba ili wapate kujifunza elimu ya ushindani lakini namna bora ya kutambua bidhaa bandia.

Sophia Kingimali
By Sophia Kingimali
04 Jul 2025
FCC YATOA ELIMU YA UTAMBUZI BIDHAA FEKI SABASABA.

Kaimu mkurugenzi mkuu wa tume ya ushindani (FCC) Tanzania bi.Hadija  Ngasongwa ametoa rai wa watanzania kujitokeza kwa wingi kwenye banda lao lililopo katika maonesho ya biashara sabasaba ili wapate kujifunza elimu ya ushindani lakini namna bora ya kutambua bidhaa bandia.

Pia amewataka wawekezaji nchini kujitokeza ili kujifunza na kuzijua sheria zinazosimamia uwekezaji nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari  leo tarehe 4 julai 2025 alipofanya ziara kwenye banda la viwanda na biashara katika maonyesho ya 49 ya biashara sabasaba amesema wawekezaji wa ndani ya nchi wanasimamiwa na sheria madhubuti zinazosimamia uwekezaji nchini, kusaidia kuimarisha biashara nchini.

" sisi tupo hapa kutekeleza kuendeleza na kutimiza azma ya Rais wa jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha hali ya biashara nchini Tanzania " amesema bi. Hadija 

Aidha amesistiza lengo la kuanzishwa  tume ya ushindani ni kusimamia na kuhimarisha ufanyaji wa biashara nchini, kulinda na kuhimarisha walaji dhidi ya mienendo potofu ya hali ya ufanyaji biashara nchini kati ya kampuni na kampuni, pamoja na kudhibiti bidhaa bandia.

Awali bi. Hadija Juma amesema lengo kubwa ni kuhakikisha  uwekezaji ndani ya nchi waone kwamba kunasheria madhubuti ambazo zitawalinda na kusimamia uwekezaji wao wanaofanya.

" Tunajivunia na tunashukuru sana serikali kuweza kutengeneza mazingira sahihi ya wawekezaji kuhakikisha kwamba mwekezaji wa ndani kuweza kupata fursa zinazopatikana na ufanyaji wa biashara na mazingira mazuri yaliyowekwa katika serikali yetu" amesema  Hadija

Pia ameongezea wameweza kushiriki katika maonyesho ya sabasaba ni fahari kwao na kuwaomba wageni wanaopita kwenye maonyesho kuchukua fursa zaidi ya makampuni 3000 yanayopatikana kwenye banda la viwanda na biashara.

Mwenye mtaji mdogo anaweza kupata fursa kuungana na mwenye kipato kikubwa au mwenye uwekezaji mkubwa na kuweza kuhimarisha biashara 

Aidha amesistiza kuna sheria ambayo ya kudhibiti bidhaa bandia, ni kosa la jinai kujihusisha na bidhaa bandia hivyo wananchi wafike kwenye banda la viwanda na biashara ili waweze kutofautisha bidhaa bandia na halisi kwa sababu kuna wataalamu wanatoa elimu.

BODI YA MKONGE TANZANIA YATANGAZA FURSA  KWA WATANZANIA.

BODI YA MKONGE TANZANIA YATANGAZA FURSA KWA WATANZANIA.

DCEA:SERIKALI IMEPUNGUZA KASI YA WALAIBU WA DAWA ZA KULEVYA.

DCEA:SERIKALI IMEPUNGUZA KASI YA WALAIBU WA DAWA ZA KULEVYA.

VITONGOJI VYOTE 64,359 VITAKUWA NA UMEME IFIKAPO 2030

VITONGOJI VYOTE 64,359 VITAKUWA NA UMEME IFIKAPO 2030

Prof.MTAMBO APONGEZA MAANDALIZI YA SABASABA 2025.

Prof.MTAMBO APONGEZA MAANDALIZI YA SABASABA 2025.