

Sekta ya Madini imechangia katika fedha za kigeni kwa mauzo yote ya bidhaa nje ya nchi kutoka Dola za Marekani bilioni 3.1 mwaka 21 hadi kufikia Dola za marekani bilioni 3.55 sawa na asilimia 46.1 huku katika bidha zisizo asili sekta ya madini imeongezeka mauzo hadi asilimia 56.2 mwaka 2023 kutoka asilimia 53.8 mwaka 2021.
Hayo yameelezwa leo Mei 15,2025 jijini hapa Dodoma na Waziri wa Madini Mhe.Anthony Mavunde wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka minne ya serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe.Dtk.Samia Suluhu Hassan.
Aidha amesema Wizara imeendelea kutekeleza maelekezo ya Serikali ya kuzalisha ajira zaidi kwa Watanzania kutoka kwenye kampuni mbalimbali za uchimbaji madini ambapo katika kipindi cha mwaka 2021 hadi 2023 Kampuni za uchimbaji madini ziliweza kuzalisha Ajira 19,356 kati ya hizoAjira 18,853 sa na asilimia 97.40 ni watanzania.
"katika kipindi hicho jumla ya bidhaa zenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 3.9 ziliuzwa na kusambazwa migodini ambapo kati ya hizo Kampuni za Watanzania zilifanikiwa kuuza bidhaa zenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 3.5 sawa na asilimia 92 ya thamani ya mauzo ya bidhaa zote na huduma zilizotolewa migodini,"amesema.
Hata hivyo amesema Mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita katika sekta hiyo yametokana na uongozi makini wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Aidha Wizara ya Madini kupitia Tume ya Madini imeendelea kutenga maeneo mahsusi kwa ajili ya wachimbaji wadogo ambapo hadi kufikia Machi 2025 maeneo 58 yametengwa katika mikoa ya kimadini ya Geita, Mara, Mbogwe, Kahama, Chunya na Songwe.
Amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango wa shughuli za uchimbaji mdogo nchini katika kutoa ajira, kuboresha kipato cha mtu mmoja mmoja na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla.
Ameeleza kuwa Serikali ya awamu ya sita imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali za kuboresha shughuli za uchimbaji mdogo nchini na kwamba kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) imefanikiwa kununua mitambo 15 ya uchorongaji miamba kwa ajili ya kutoa huduma kwa wachimbaji wadogo.
Waziri Mavunde amesema kufuatia ununuzi wa mitambo hiyo, STAMICO imeendelea kutoa huduma ya uchorongaji kwa bei nafuu kwa wachimbaji wadogo.
"Katika kipindi husika wachimbaji wadogo 16 tayari wamepata huduma hii katika maeneo ya Tambi – Mpwapwa, Nyawa – Bariadi, Matondo, Makongolosi na Matundasi – Chunya, Lwamgasa, Nyaruyeye, Nyamalimbe na Nyakagwe – Geita, Mavota – Biharamulo, Endabash – Karatu, Mwakitolyo – Shinyanga na Mbangala - Songwe," alisema.
Ameongeza kuwa katika utekelezaji huo, jumla ya mita 3,450.37 zimechorongwa katika maeneo hayo huku akisema Wizara kupitia STAMICO imeendelea kuratibu shughuli za uchimbaji mdogo kwa kutoa huduma za kitaalamu kwa wachimbaji wadogo katika nyanja za utafiti, uchimbaji, uchenjuaji madini pamoja na utunzaji wa mazingira.
Waziri huyo ameeleza jumla ya wachimbaji wadogo 471 wamepatiwa mafunzo kupitia vituo vya mfano vya Katente, Lwamgasa na Itumbi ambapo mpaka sasa wachimbaji 12 wa madini wameanzisha vituo vyao baada ya kujifunza kupitia vituo hivyo.
Aidha, amefafanua kuwa kupitia vituo hivyo vya mfano, huduma ya uchenjuaji mbale za dhahabu kwa wateja 41 ilitolewa ambapo dhahabu ya uzito wa kilogramu 119.57 yenye thamani ya Shilingi 23,318,849,170.45 ilichenjuliwa.
Sekta ya Madini ni miongoni mwa sekta muhimu katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya kijamii na Taifa kwa ujumla.
PPAA yatoa elimu matumizi ya Moduli Wiki ya Utumishi wa Umma
KIHENZILE: UWAZI NA UWAJIBIKAJI NI NGUZO MUHIMU ZENYE TIJA KWA WANANCHI
KIHENZILE:WIKI YA UTUMISHI WA UMMA NI FURSA MUHIMU KWA WANANCHI
ACT WAZALENDO KUUWASHA MOTO MANZESE WAJIDHATITI KUCHUKUA MAJIMBO YOTE DAR ES SALAAM
TANESCO YAJA NA KAMPENI MAALUM YA KUHAMASISHA ULIPAJI WA MADENI KWA WATEJA.
DODOMA YAELEKEA IRINGA KWA KISHINDO MASHINDANO YA UMISSETA.
Serikali Yatangaza Kuanza Msako Kuwabaini Wanaotumikisha Watoto
GRAND BUNGE BONANZA KUFANYIKA JUNI 21 2025 HUKU MGENI RASMI AKITARAJIWA KUWA RAIS SAMIA.
MOI YASEMA WAGONJWA WENGI WANAOWAHUDUMIA WANA MATATIZO SUGU.
NISHATI YA GESI ASILIA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA NCHI.