
Hayo yamejiri Kufuatia wakazi wa maeneo mbalimbali hapa nchi kutochukua tahadhari za mara kwa mara katika kujilinda na wanyama wakali ambao ni hatarishi kwa maisha yao.
Beatus Maganja ambae ni Afisa Habari mamlaka ya Usimamizi wanyama Pori Tanzania TAWA amewaeleza wananchi hao kuwa serikali imejipanga kikamilifu ili kuhakikisha wananchi wanakuwa salama.
"katika kukabiliana na changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu Serikali inahakikisha usalama wa mwananchi unakuwa ni kipaumbele cha kwanza na ndiyo maana mara kwa mara Maofisa wa TAWA wamekuwepo maeneo mbalimbali nchini kutoa elimu na kufanya doria katika maeneo ambayo yanatajwa kuwa na changamoto ya wanyamapori hao". Amesema hayo Maganja.
Kwa upande Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Bw. Joshua Manumbu ameipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA kwa elimu wanayoendelea kuitoa katika jamii namna ya kuepuka madhara yanayoweza kusababishwa na wanyamapori wakali na waharibifu hususani mamba na viboko na kuwadhibiti pale wanapoonekana kuhatarisha maisha ya wananchi.
"Halmashauri ya wilaya ya Ukerewe imekuwa ikifanya kazi kwa ukaribu na Maofisa wa TAWA kutoka Kanda Maalumu ya Mwanza na imetoa ushirikiano mkubwa kwa Maofisa hao ili kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo" .amesema hayo Manumbu
Kwa upande wao, wananchi wa Kijiji cha Selema kilochopo Kata ya Bwiro wilayani humo wameipongeza na kuishukuru TAWA kwa elimu wanayoendelea kuitoa wilayani humo ambayo wamekiri kuwa imekuwa msaada kwao na itawawezesha kuendelea na shughuli zao za kiuchumi huku wakiepuka madhara yanayoweza kusababishwa na wanyamapori hao.
Mamlaka ya usimamizi wanyamapori Tanzania TAWA imekuwa ikitoa elmu maeneo mbalimbali hapa nchini lengo ikiwa ni kuwafikia wananchi wanaoishi maeneo hatarishi dhidi ya wanyama hao.
PPAA yatoa elimu matumizi ya Moduli Wiki ya Utumishi wa Umma
KIHENZILE: UWAZI NA UWAJIBIKAJI NI NGUZO MUHIMU ZENYE TIJA KWA WANANCHI
KIHENZILE:WIKI YA UTUMISHI WA UMMA NI FURSA MUHIMU KWA WANANCHI
ACT WAZALENDO KUUWASHA MOTO MANZESE WAJIDHATITI KUCHUKUA MAJIMBO YOTE DAR ES SALAAM
TANESCO YAJA NA KAMPENI MAALUM YA KUHAMASISHA ULIPAJI WA MADENI KWA WATEJA.
DODOMA YAELEKEA IRINGA KWA KISHINDO MASHINDANO YA UMISSETA.
Serikali Yatangaza Kuanza Msako Kuwabaini Wanaotumikisha Watoto
GRAND BUNGE BONANZA KUFANYIKA JUNI 21 2025 HUKU MGENI RASMI AKITARAJIWA KUWA RAIS SAMIA.
MOI YASEMA WAGONJWA WENGI WANAOWAHUDUMIA WANA MATATIZO SUGU.
NISHATI YA GESI ASILIA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA NCHI.